Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zinedine Zidane kurudi mzigoni

ZIDANE Pict

Muktasari:

  • Zidane, 52, amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Real Madrid 2021, aliporejea kwenye kikosi hicho mara ya pili baada ya mwanzoni kuondoka. Kocha huyo Mfaransa amekuwa hana kazi licha ya kushinda La Liga mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo alipokuwa Real Madrid katika awamu zake mbili alizoionoa miamba hiyo ya Bernabeu.

MADRID, HISPANIA: HABARI ndo hiyo. Zinedine Zidane atarejea kwenye kazi ya ukocha kwenye timu mbili tu na bahati mbaya hakuna hata moja ya Ligi Kuu England. Mmesikia mashabiki mnaomtaka kumwona Zidane kwenye Ligi Kuu England?

Zidane, 52, amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Real Madrid 2021, aliporejea kwenye kikosi hicho mara ya pili baada ya mwanzoni kuondoka. Kocha huyo Mfaransa amekuwa hana kazi licha ya kushinda La Liga mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo alipokuwa Real Madrid katika awamu zake mbili alizoionoa miamba hiyo ya Bernabeu.

Na si kwamba Zidane hakuwa anapata ofa katika kipindi hicho cha miaka mitatu aliyokuwa hana ajira, lakini ame-zigomea nyingi tu.

Zizou alifuatwa na klabu kubwa duniani, ikiwamo Manchester United, Bayern Munich, Juventus na Paris Saint-Germain.

Kuna timu za taifa kadhaa nazo zilimfuata mshindi huyo wa Ballon d’Or 1998 ili akazinoe, lakini nazo alizigomea.

Kwa mujibu wa Marca, Zidane amekuwa hana kazi kwa muda wote huo kwa sababu, yeye anachotaka ni kufanya kazi kwenye timu mbili tu, kama sio Real Madrid basi ni timu ya taifa ya Ufaransa, Les Bleus. Sababu kubwa ya hilo ni kwamba Zidane amekuwa mtiifu sana kwenye timu hizo, akiamini hawezi kufanya kazi kwenye timu nyingine zaidi ya kipezi chake Los Blancos na Tricolores. Ripoti hiyo ilibainisha kwamba, kitu ambacho kitaweza kubadili msimamo wa Zidane ni kuwapo na klabu itakayokuwa na mipango madhubuti. Lakini, kwa sasa, inaelezwa ni ngumu kumwona Mfaransa huyo kwenye benchi la ufundi la klabu nyingine.

Mtaliano, Carlo Ancelotti kwa sasa ndiye kocha wa Real Madrid, ambao ni mabingwa mara 36 wa La Liga na mara 15 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na huko kwenye kikosi cha Ufaransa, staa wa zamani wa timu hiyo, Didier Deschamps anaendelea kuinoa baada ya kusaini mkataba mpya hadi 2026, wakati wa fainali za Kombe la Dunia huko Amerika.

Huko nyuma iliwahi kuelezwa kwamba Zidane atapenda kufanya kazi kwenye nchi ambayo inazungumza lugha anayoifahamu vyema, hiyo ina maana ni Hispania na Ufaransa pekee. Kwenye kazi ya ukocha, Zidane alianza Juni 2014 alipochukua mikoba ya kuinoa Real Madrid B.

Alitumikia kwa miezi 18 kabla ya kupewa mikoba e timu ya wakubwa baada ya Rafael Benitez kufutwa kazi.

Zidane mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa cha Real Madrid ilikuwa Januari 2016 na aliwaongoza kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili. Lakini, mambo yalikuwa matamu  Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo aliisaidia kunyakua taji lao la 11 la Ulaya kwa mikwaju ya penalti dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid.

Zidane, ambaye ni staa wa zamani wa Los Blancos mambo yake yalikuwa mazuri kwenye La Liga kwenye msimu wa 2016-17, huku akiiongoza kubeba pia taji la Uefa Super Cup na Club World Cup. Taji lake la pili mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya lilifuatia pia baada ya Real Madrid kuichapa Juventus kwenye fainali ya michuano hiyo iliyofanyika uwanjani Principality.

Zidane aliandika historia msimu uliofuatia wakati alipokuwa kocha wa kwanza kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali na hapo Los Blancos iliandika historia pia ya kuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa tatu mfululizo.

Zidane alitangaza kung’atuka Real Madrid siku tano baadaye baada ya fainali, akidai klabu ilihitaji kuchukua njia tofauti. Alirejea kwenye kikosi hicho cha Bernabeu, Machi 2019 baada ya Santiago Solari na Julen Lopetegui kuiongoza timu hiyo kwa muda mfupi.