Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Mgunda Simba lipo hivi, Mashujaa waweka masharti


KUNA taarifa zinaeleza kwamba, Simba ipo katika hatua nzuri ya kumsajili mshambuliaji Ismail Mgunda kutoka Mashujaa ikiwa ni mbadala wa Selemani Mwalimu aliyejiunga na Yanga.


Taarifa kutoka katika kambi ya Mashujaa zinabainisha kwamba, mshambuliaji huyo ameondoka na ku-tua Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Mgunda ambaye msimu uliopita alifunga mabao mawili na asisti moja katika Ligi Kuu Bara, mara kadhaa amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba, hivyo kuna uwezekano mkubwa msimu wa 2026-2027 aka-vaa jezi za Wanamsimbazi.

Chanzo kutoka Mashujaa kilibainisha kwamba, kufuatia Mgunda kupata taarifa za kutakiwa na Simba, uongozi wa klabu ulifikia uamuzi wa kumtoa kambini ili kumpa utulivu na kwenda kukamilisha dili hilo.

“Tumemuondoka mchezaji kambini ili kumpa muda wa kutulia zaidi na kukamilisha dili hilo, tunacho-subiri ni Simba kuweka fedha tulizokubaliana ili mchezaji awe mali yao. Wakiweka muda wowote, suala la kumtambulisha litakuwa la kwao kwani biashara itakuwa imefanyika,” kilisema chanzo.

Chanzo hicho hakijaweka wazi ni kiasi gani cha fedha wamekubaliana Mashujaa na Simba kwa ajili ya dili hilo, huku ikibainisha kwamba mshambuliaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Mgunda kabla ya kuitumikia Mashujaa, msimu wa 2024-2025 alikuwa AS Vita ya DR Congo, huku 2023-2024 akiitumikia Singida BS akifunga mabao sita.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa Mashujaa, alisema dili la Mgunda kwenda Simba, wao hawana shida, kikubwa ni makubaliano kwani bado mshambuliaji huyo ana mkataba klabuni hapo.

Uamuzi wa Simba kumuhitaji Mgunda, umetokana na Mwalimu aliyeichezea klabu hiyo msimu uliopita kwa mkopo kutoka Wydad AC kuibukia Yanga.

Katika hatua nyingine, Simba imetajwa kuwa katika harakati za kumsajili mshambuaji Paul Peter kutoka JKT Tanzania.