Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bihina shujaa wa Cameroon WAFCON

Muktasari:

  • Bihina, ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kuwatoa Nigeria katika robo fainali kwa kufanya sevu tisa, alikuwa na kiwango bora dhidi ya Morocco akizuia penalti ikiwemo ya Fatima Tagnaout katika dakika za nyongeza kabla ya kuokoa mikwaju ya Kenza Chapelle, Maryame Atiq na Sakina Diki Ouzraoui katika changamoto ya mikwaju ya penalti.

KIPA wa Cameroon, Michaely Bihina, ameendelea kuwa shujaa wa WAFCON 2026 baada ya kuisaidia timu hiyo kuwatupa nje wenyeji Morocco kwa mikwaju ya penalti 3-1 kufuatia suluhu katika dakika 120.

Bihina, ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kuwatoa Nigeria katika robo fainali kwa kufanya sevu tisa, alikuwa na kiwango bora dhidi ya Morocco akizuia penalti ikiwemo ya Fatima Tagnaout katika dakika za nyongeza kabla ya kuokoa mikwaju ya Kenza Chapelle, Maryame Atiq na Sakina Diki Ouzraoui katika changamoto ya mikwaju ya penalti.

Morocco ilianza mchezo kwa kasi na kutawala, lakini Cameroon iliweka ukuta imara mbele ya lango lake. Sakina Ouzraoui na Hanane Aït El Haj walitengeneza nafasi nyingi upande wa kulia, huku Bihina na safu yake ya ulinzi ikifanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi hayo.

Kipindi cha pili Morocco iliongeza presha, lakini Bihina aliendelea kuwa kikwazo kikubwa. Kipa huyo mwenye miaka 22 alionyesha tena uwezo wake na ujasiri mkubwa, akitoka langoni kwake katika mazingira magumu na kuudaka mpira mbele ya wachezaji kadhaa wa Morocco.

Dakika ya 90+3, Morocco ilipata nafasi kubwa ya kuvunja mwiko baada ya Ouzraoui kupenya kuelekea langoni, lakini Bihina alitoka kwa wakati na kuokoa. Mpira ukaenda upande mwingine na Cameroon ikapata nafasi kupitia Michaela-Batya Abam, lakini shuti lake likaenda juu ya lango, mchezo ukiingia muda wa nyongeza bila bao.

Akizungumza baada ya kiwango hicho, Bihina amesema ushindi huo ulikuwa wa kihistoria kwake na kwa kizazi kipya cha timu ya taifa ya Cameroon.

“Nimefurahi sana kwa sababu mimi ni sehemu ya kizazi kipya cha timu yetu ya taifa. Tunaijua Nigeria, Morocco na timu zingine kila mara imekuwa ikizifunga Cameroon, lakini tuliamua kubadilisha mambo. Motisha hiyo ilitusaidia sana,” amesema.

Kipa huyo amesema kabla ya mchezo kocha aliwaambia wachezaji kwamba walikuwa na dakika 90 pekee za kuamua hatma ya kutinga fainali.

“Kabla hatujaingia uwanjani, kocha alituambia kwamba tunapaswa kutengeneza historia, kwamba tulikuwa tumebakiza dakika 90 tu kufuzu Kombe la Dunia. Ama tuamue kwenda Brazil au turudi nyumbani,” amesema Bihina.

Hii ni fainali ya tano kwa Cameroon na mara nne ilizocheza, ilimaliza nafasi ya pili.