Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dau lililompeleka Mgunda Simba


SIMBA imekamilisha usajili wa mshambuliaji Ismail Mgunda baada ya kununua mkataba wa mwaka mmoja kutoka Mashujaa, huku ikielezwa kuwa, zaidi ya Sh100 milioni zimetumika kufanikisha dili hilo.


Chanzo kutoka Mashujaa kimesema, Simba imetoa kiasi hicho cha fedha ili kuvunja mkataba wa Mgunda na tayari kila kitu kimekamilika, kilichobaki ni mshambuliaji huyo kutangazwa.

"Siwezi kukutajia dau moja kwa moja lakini elewa kwamba Simba imetoa zaidi ya Sh100 milioni, kwa sasa Mgunda siyo mchezaji wetu, ni mali ya Simba, tunamtakia majukumu mema ya timu anayokwenda kuichezea," kimesema chanzo hicho na kuongeza;

"Simba ilianza kuhitaji huduma ya Mgunda kwa muda mrefu lakini nadhani wakati huu ndiyo ulikuwa muda wake sahihi kumsajili, ni mchezaji mwenye nidhamu ya hali ya juu, anajitambua na anajua anataka nini na afanye kwa wakati gani."

Kwa upande wa Simba, chanzo kimesema usajili wa Mgunda ni kwenda kuziba nafasi ya Seleman Mwalimu aliyetua Yanga, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kupata mshambuliaji mwingine zaidi.

"Tunaweza tukaongeza wachezaji wengine, tunaangalia uwezekano lakini lolote linaweza likatokea," kimesema chanzo hicho.

Mgunda ambaye sasa ana jukumu la kwenda kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji la Simba, msimu wa 2023-2024 alifunga mabao sita akiwa na Singida Black Stars, kisha 2024-2025 akaenda kucheza Ligi ya DR Congo katika klabu ya AS Vita, akarejea nchini na kuitumikia Mashujaa alipomaliza msimu wa 2025-2026 akifunga mabao mawili ya Ligi Kuu Bara.

Lakini kwa upande wa Mwalimu ambaye msimu uliopita alimaliza na mabao tisa na asisti moja ya ligi kuu, msimu wa 2024-2025 kabla ya kwenda Wydad Casablanca, alifunga mabao sita akiwa na Fountain Gate.