Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yametimia huko! Sesko atua rasmi Man United

CHUMA Pict

Muktasari:

  • Man United imetangaza Sesko, 22, amejiunga kwa mkataba wa miaka mitano kutoka kwenye klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig kwa ada ya Pauni 74 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA, Benjamin Sesko ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Manchester United baada ya miamba hiyo ya Old Trafford kushinda vita ya kunasa saini yake dhidi ya Newcastle United.

Man United imetangaza Sesko, 22, amejiunga kwa mkataba wa miaka mitano kutoka kwenye klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig kwa ada ya Pauni 74 milioni.

Straika huyo alikuwa kwenye rada za timu nyingi za Ulaya kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, ikiwamo mahasimu wa Man United, Arsenal kabla ya kumsajili straika mwingine, Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon.

Lakini, walikuwa Man United na Newcastle ndizo zilizokuwa zikichuana kuwania saini ya straika huyo wa kimataifa wa Slovania hadi mwisho, mchezaji mwenyewe alipochagua kwenda Old Trafford na kukacha fursa ya kwenda kukipiga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huko St James' Park.

Baada ya kutua Theatre of Dreams, Sesko alisema: "Historia ya Manchester United ni kitu spesho, lakini kilichonivutia hapa ni mipango yao ya baadaye.

  • CHU 01

“Tulipozungumza juu ya mipango yao, kila kitu kilijipambanua kwamba hii timu inaendelea kukua na imelenga kupambana kwenye mataji makubwa tena.

“Tangu nilipowasili, nimeona hapa mzuka chanya na mazingira mazuri ambayo klabu imeyaandaa. Ni dhahiri ni mahali sahihi kwangu mimi kufikia viwango vyake na kufikia malengo.

“Nasubiri kwa hamu kuanza kujifunza kutoka kwa kocha Ruben Amorim na kujumuika na wachezaji wangu kufikia mafanikio ambayo tunafahamu wazi tutayafikia kwa pamoja.”

CHU 05

Sesko alitamba sana kwenye Bundesliga msimu uliopita, wakati alipofunga mabao 13 na kuasisti mara tano katika mechi 33. Na sasa atakwenda kuungana na wachezaji wenzake wapya waliosajiliwa dirisha hili, Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwenye safu mpya ya ushambuliaji ya kocha Amorim kwa ajili ya msimu huu, ambapo mabosi wa Man United wamelenga kuilata timu kivingine.

CHU 02

Ripoti zinafichua, Sesko atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 160,000 kwa wiki, mkwanja ambao utamfanya kushika namba nane kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa vizuri kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Mshahara wa Sesko utaongezeka na kufikia Pauni 200,000 kwa wiki, endapo kama Man United itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwenye dau la Pauni 74 milioni, Man United itatanguliza kulipa Pauni 66.5 milioni na Pauni 7.3 milioni za ziada zitalipwa kama bonasi, huku malipo hayo yakiwekwa kwenye mfumo ambao Man United walihitaji.

Sesko amekuwa akisifiwa kwa kucheza soka la nguvu, kumiliki mpira na kasi na umaliziaji mzuri huku akiwa na uwezo mkubwa wa kuruka hewani kama ambavyo amekuwa akifanya supastaa Cristiano Ronaldo.

Mkurugenzi wa soka wa Man United, Jason Wilcox alisema: "Benjamin anamiliki mjumuiko wa vitu adimu kabisa, kasi na nguvu ya kuwapelekesha mabeki wa timu pinzani, hilo limemfanya kuwa mmoja wa watu tofauti kabisa kwenye orodha ya vijana wenye viwango vya dunia.

CHU 03

“Tulimfuatilia kwa karibu sana Benjamin pamoja na kuzingatia mambo yote yanayohitajika ili kumfanya awe bora hapa Manchester United. Kuwa chini ya Ruben na timu yetu bora kabisa ya viwango, Benjamin amejiunga kwenye mazingira mazuri kabisa yanayompa sapoti kufikia ubora wa dunia."

Akiwa na kimo cha urefu wa futi 6 na inchi 5, Sesko amekuwa akipata mlo mataa kabisa, ambapo kifungua kinywa chake kinahusiska mayai manne ya kukaanga, mtindi wa matunda, muesli na juisi ya matunda.

Mlo wa mchana, Sesko anakula kuku, wali, karoti na broccoli, slesi mbili za mkate pamoja na bakuli la matunda ambayo ni embe, tikiti na nanasi.

Mlo wa usiku ni samaki na viatu, nyanya na kachumbali ya tano pamoja na muesli, huku akigonga korosho na matunda mengine jamii ya dhabibu.

CHU 04

Sesko alianza maisha yake ya soka RB Salzburg kabla ya kutua Leipzig mwaka 2023. Ameitumikia timu ya taifa ya Slovenia mara 41 kwenye soka la kimataifa akifunga mara 16 na asisti sita.


MECHI 10 ZA KWANZA ZA MAN UNITED ZA EPL 2025-206

-Agosti 17 vs Arsenal (nyumbani)

-Agosti 24 vs Fulham (ugenini)

-Agosti 30 vs Burnley (nyumbani)

-Septemba 14 vs Man City (ugenini)

-Septemba 20 vs Chelsea (nyumbani)

-Septemba 27 vs Brentford (ugenini)

-Oktoba 4 vs Sunderland (nyumbani)

-Oktoba 18 vs Liverpool (ugenini)

-Oktoba 25 vs Brighton (nyumbani)

-Novemba 1 vs Nottm Forest (ugenini)