Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Fiorentina asimamisha mazoezi Wolves

TOLU Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa, nyota huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 25 aliketi katikati ya uwanja na kudai klabu imruhusu kujiunga na Fiorentina, ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

LONDON, ENGLAND: MSHAMBUALIAJI wa Wolves, Tolu Arokodare alisababisha mazoezi ya timu hiyo kusitishwa baada ya kugoma kuondoka uwanjani huku akishinikiza kuhamia Fiorentina.

Kwa mujibu wa taarifa, nyota huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 25 aliketi katikati ya uwanja na kudai klabu imruhusu kujiunga na Fiorentina, ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

Hata hivyo, Wolves imekataa ofa ya klabu hiyo ya Italia, huku ikikubali pendekezo kutoka Trabzonspor ya Uturuki.

TOL 01

Kitendo cha Arokodare kilimlazimu kocha mpya Cesar Peixoto kusitisha mazoezi ya Jumatatu, ikiwa ni changamoto ya kwanza kwake tangu atue Molineux mwezi uliopita.

Arokodare hakuwamo kwenye kikosi kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Maidenhead United Jumatano, wakati Wolves ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

TOL 03

Arokodare ajitetea

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, mshambuliaji huyo alikanusha madai ya kukosa nidhamu na kusisitiza kuwa ataendelea kutekeleza majukumu yake akiwa chini ya mkataba na Wolves.

"Katika maisha yangu yote ya soka, nimekuwa nikijivunia kuwa weledi na kufuata viwango vya juu vya mazoezi. Nitaendelea kufanya kazi yangu kwa weledi na kuchangia timu kadri nitakavyohitajika," aliandika Arokodare.

Ameongeza kuwa bado ana mkataba na Wolves na lengo lake ni kuendelea kuheshimu makubaliano hayo.

TOL 02

Hii si mara ya kwanza kwa Arokodare kuingia kwenye matatizo ya kinidhamu akiwa Wolves.

Mwezi Aprili aliwahi kuchukuliwa hatua baada ya kugombana na mshambuliaji kijana Mateus Mane.

Arokodare alisajiliwa kutoka Genk kwa pauni24 milioni msimu uliopita, lakini alifunga mabao matatu pekee ya Ligi Kuu England huku Wolves ikimaliza mkiani na kushuka daraja.

Sasa tukio hilo linakuwa mtihani wa mapema kwa Peixoto, ambaye alichukua nafasi ya Rob Edwards na amepewa jukumu la kuirejesha Wolves Ligi Kuu England katika jaribio la kwanza.