Xavi Simons anasakwa Bayern Munich
Muktasari:
- Staa huyu mwemye umri wa miaka 21, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliomalizika alicheza mechi 44 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 15.
KIUNGO wa Paris St-Germain na Uholanzi Xavi Simons ni miongoni kwa wachezaji wa kwanza ambao Bayern Munich imepanga kukamilisha usajili wao katika dirisha hili.
Staa huyu mwemye umri wa miaka 21, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliomalizika alicheza mechi 44 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 15.
ARSENAL imewasilisha ofa kwenda Fenerbahce ili kuipata saini ya beki wa pembeni wa timu hiyo na Uturuki Ferdi Kadioglu, 24, baada ya kuvutiwa na kiwango bora alicho onyesha akiwa na kikosi cha Uturuki katik michuano ya Euro.
Mkataba wa fundi huyu na Fenerbanhce unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Taarifa zinaeleza inahitajika zaidi ya Pauni 30 milioni ili kumpata.
WEST Ham na Nottingham Forest zimetuma email kwa Arsenal kuomba kufanya nao mazungumzo kwa ajili ua kuipata saini ya kiungo wao, Reiss Nelson katika dirisha hili.
Baada ya kumalizika msimu huu, tetesi zimekuwa zikieleza kwamba Arsenal imepanga kuwauza baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza na mmoja wao ni Reiss.
Mkataba wa kiungo huyu unamalizika mwaka 2027.
RIPOTI kutoka tovuti ya The Athletic inaeleza kuwa Arsenal na Chelsea zipo katika mazungumzo na Athletic Bilbao kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na Hispania, Nico Williams katika dirisha hili.
Inaelezwa staa huyo katika mkataba wake kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Euro 55 milioni.
NICOLO Zaniolo yupo kwenye rada za timu mbalimbali za Italia ikiwemo Atalanta na Fiorentina ambazo kwa sasa zipo katika vita kali ya kuiwania huduma yake.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari kutoka Italia, Gianluca Di Marzio timu inayopewa nafasi kubwa ya kumpata staa huyu wa Galatasaray ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Aston Villa ni Atalanta.
Masimu uliopita alicheza mechi 25 za Ligi Kuu England na kufunga mabao mawili.
LEEDS inaonekana kushindana jino kwa jino na Leicester City katika vita ya kuiwania saini ya beki wa Tottenham na Wales, Joe Radon ambaye pia anawindwa na Southampton na Ipswich Town, zote zikihitaji kumsajili, katika dirisha hili.
Radon hajapata nafasi kubwa ya kucheza kwa msimu uliopita na hiyo ndio imesababisha awasilishe barua ya kuomba kuondoka kwa mkopo au auzwe mazima kwa ajili ya kwenda timu itakayompa nafasi kubwa ya kucheza ili kulinda kipaji chake.
TOTTENHAM imefikia patamu katika mazungumzo yao na Bologna juu ya kumsajili beki wa timu hiyo na Italia, Riccardo Calafiori katika dirisha hili.
Calafiori, 22, pia huduma yake inahitajika na Juventus ambayo imeshaanza mazungumzo ili kumsajili staa huyo aliyekuwa chachu ya kufanya vizuri kwa Bologna kwa msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Italia.
Bologna imeripotiwa kuhitaji zaidi ya Euro 50 milioni ili kumuuza.