Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wikiendi ya ngumi: Fury, Joshua kukiwasha

MASUMBWI Pict

Muktasari:

  • Fury ndiye atakayefungua pazia la mapambano hayo leo Ijumaa kwa kumenyana na Mariusz Wach nchini Thailand katika pambano la kujipima nguvu kabla ya pambano lake kubwa dhidi ya Anthony Joshua litakalofanyika Novemba mwaka huu.

JEDDAH, SAUDI ARABIA: MABONDIA wenye hadhi ya juu duniani wataingia ulingoni leo na kesho kwa Tyson Fury, Anthony Joshua, Tim Tszyu na Errol Spence Jr watashuka ulingoni katika mapambano yanayosubiriwa kwa hamu.

Fury ndiye atakayefungua pazia la mapambano hayo leo Ijumaa kwa kumenyana na Mariusz Wach nchini Thailand katika pambano la kujipima nguvu kabla ya pambano lake kubwa dhidi ya Anthony Joshua litakalofanyika Novemba mwaka huu.

Siku moja baadaye, Joshua atarejea ulingoni kwa kumkabili Kristian Prenga mjini Jeddah, Saudi Arabia, huku nchini Australia mabingwa wa zamani wa dunia Tim Tszyu na Errol Spence Jr. wakitarajiwa kukutana katika pambano kubwa la uzani wa middleweight litakalopigwa Sydney.

MASU 01

FURY AJINOA KABLA YA JOSHUA

Mapambano dhidi ya Wach yanachukuliwa kama maandalizi muhimu kwa Fury kuelekea pambano lake linalosubiriwa kwa hamu dhidi ya Joshua, ambalo linatarajiwa kuwa miongoni mwa mapambano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya ngumi za Uingereza.

Fury mwenye umri wa miaka 37, atapambana na Mpoland Mariusz Wach mjini Pattaya, Thailand, huku mpinzani huyo mwenye miaka 46 akitarajiwa kuwa wa mwisho kumkabili kabla ya pambano kubwa la Waingereza hao wawili maarufu kama "Battle of Britain."

Tofauti na ilivyozoeleka, pambano hilo litafanyika bila mashabiki  nchini Thailand na halitarushwa mubashara kwenye televisheni.

Tofauti na ilivyozoeleka, pambano hilo litafanyika bila mashabiki na halitarushwa mubashara na kituo chochote cha televisheni, isipokuwa kama kutatokea mabadiliko ya dakika za mwisho.

Kampuni ya Netflix kwa sasa inaandaa msimu wa tatu wa filamu ya kumbukumbu At Home with the Furys, huku picha za pambano hilo dhidi ya Wach zikitarajiwa kuwa sehemu ya maudhui yatakayoonyeshwa msimu huo utakapozinduliwa.

Netflix pia ndiyo yenye haki za kurusha pambano la Fury dhidi ya Joshua iwapo litafanyika kama ilivyopangwa.

MASU 02

JOSHUA APANDA ULINGONI SIKU INAYOFUATA

Pambano la Fury litafanyika usiku mmoja kabla ya Joshua kumenyana na Kristian Prenga wa Albania mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Tofauti na pambano la Fury, mpambano wa Joshua utarushwa mubashara kupitia DAZN PPV.

Kutokana na tofauti ya siku moja kati ya mapambano hayo mawili, kuna uwezekano Fury akasafiri hadi Saudi Arabia kushuhudia pambano la Joshua akiwa karibu kuanza maandalizi ya mwisho ya pambano lao kubwa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Joshua mwenye umri wa miaka 36, alipigana mara ya mwisho mwezi Desemba mwaka jana alipomchapa Jake Paul kwa knockout ya raundi ya sita mjini Miami.

Kwa upande wa Prenga, mwenye miaka 35, anafahamika kwa nguvu zake za kupiga knockout, lakini hajawahi kujijengea jina kama mpinzani wa kiwango cha dunia katika uzani wa juu.

Swali kubwa ni je, Joshua ataendelea na ushindi utakaomuweka kwenye njia ya pambano dhidi ya Fury, au Prenga atafanya maajabu kwa kuibuka na ushindi wa kushtua?


JOSHUA ALIVYOTENGENEZA HISTORIA

Joshua alianza kung'ara baada ya kutwaa medali ya dhahabu ya Olimpiki ya London 2012, kabla ya kugeuka bondia wa kulipwa mwaka uliofuata.

Alishinda mapambano yake 16 ya kwanza kwa knockout, mfululizo uliomfikisha kwenye ubingwa wa dunia wa IBF baada ya kumshinda Charles Martin.

Mwaka 2017, Joshua aliandika historia kwa kumchapa Wladimir Klitschko kwa knockout ya raundi ya 11 katika Uwanja wa Wembley na kuunganisha mikanda ya IBF na WBA.

Mwaka mmoja baadaye alimshinda Joseph Parker kwa uamuzi wa majaji na kuongeza mkanda wa WBO kwenye mkusanyiko wake.

Joshua alipata kipigo chake cha kwanza mwaka 2019 dhidi ya Andy Ruiz Jr, lakini alilipiza kisasi katika pambano la marudiano na kurejesha mikanda yake.

Baadaye alipoteza mara mbili mfululizo dhidi ya Oleksandr Usyk mwaka 2021 na 2022, kabla ya kurejea kwa ushindi wa mapambano manne mfululizo uliompa nafasi ya kuwania kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu.

Hata hivyo, mwaka 2024 alizimwa na Daniel Dubois, aliyemchapa kwa knockout ya raundi ya sita na kutetea mkanda wa IBF.

Joshua alirejea tena Desemba 2025 kwa ushindi wa knockout dhidi ya Jake Paul, na sasa ana rekodi ya ushindi 29 na vipigo vinne, huku 26 kati ya ushindi huo akiwa amepata kwa knockout.

MASU 03

PRENGA ANATEGEMEA NGUVU ZA KNOCKOUT

Prenga alianza ngumi za kulipwa miaka mitatu baada ya Joshua na alishinda mapambano yake manne ya kwanza kwa knockout.

Alipoteza pambano lake la tano, ambalo ndilo pekee alilowahi kushindwa katika maisha yake ya ngumi.

Tangu wakati huo ameandika ushindi 16 mfululizo, ingawa hajawahi kupambana na majina makubwa katika uzani wa juu.

Hata hivyo, Prenga ni bondia hatari kutokana na uwezo wake wa kumaliza mapambano mapema, akiwa amepata ushindi wake wote 20 kwa knockout, jambo linalomfanya kuwa tishio kwa Joshua.