Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri imefichuka! Mazito yanayomfanya Tabu Mtingita atoe chozi

KAMERA Pict


USTAA unatambulisha kipaji cha mtu, lakini haumaanishi anaweza akaishi kama malaika kuna wakati nje na macho ya jamii wanalia na kupitia mambo magumu kama watu wengine.


Nyuma ya Kamera imepata nafasi ya kupiga stori za hapa na pale na mchekeshaji mahiri wa kike nchini, Tabu Mtingita anasimulia matukio anayopigwa kwenye mahusiano pamoja na umaarufu wake, huku akisisitiza jamii inapaswa kuelewa kwamba na wao ni binadamu wana nyama na wanapumua pumzi moja ya Mwenyezi Mungu.


Anajitolea mfano namna anavyoumia, licha ya kuwa mwanamke anayejali na kujua jinsi ya kumtunza mwanaume, lakini bado kuna muda anaona usaliti unaomuumiza.

“Mfano kama mimi napigwa matukio hadi mwili unauma, licha ya kuvumilia vitu vikubwa vya kuumiza ili mradi muweze kufika mbali, kumbe mwenzako anakuwa mguu pande mguu sawa,” anasema Tabu na kuongeza;

“Mfano huyo Mtaribani au Kiposongo wangu (mwenza wake), ningemchungulia kwenye moyo wake na kuona amekaa kwenye mstari mwekundu unaghairi, ila unakuwa hujui maana unakuwa unatumia muda wako mwingi kupanga malengo kumbe ana malengo mengine kichwani mwake.”

KAME 01

Anasimulia tukio lililomuumiza ni kufuma ujumbe uliotumwa kwa maandishi (meseji) katika simu ya mwenza wake, ulioandikwa na mwanamke mwingine ukisema aachane na Tabu ni kibonge.

“Unaweza ukaona meseji ukakausha ukaenda kulilia chooni, hiyo inauma sana asikwambie mtu, kipindi hiki nipo katika kuvumilia, ila nitakaposhindwa uzuri naweka wazi kwamba nimependa au nimeacha,” anasema na kuongeza;

“Baada ya kusoma meseji ya mpenzi wake inayosema achana na Tabu huyo ni kibonge, nilivunja TV inchi 45, niliitoa ukutani na kuibwaga chini, ilinichukua mwezi kumsamehe, nilikuwa napika anakula lakini moyoni mwangu nilikuwa natamani kumkaba, lakini niliomba subira ya Mwenyezi Mungu na nikaamua kununua vitu vingine, maana mbali na tv nilivunja vingine vidogovidogo.”

KAME 02

Anasema imekuwa ngumu kwa watu maarufu kupata wenza wenye upendo wa kweli, wengi wao wanachukulia maisha ya muvi na kuona yamebeba uhalisia. “Wanaokuja katika maisha yetu hudhani kila mtu ana mapichapicha, tunayoyafanya kwenye sinema wanadhani yapo hadi kwenye majumba yetu, hivyo wanajua leo nina tabu atakaponitambulisha kwa wasanii wengine ambao pengine ni wazuri kuliko mimi, atakuacha na kuwa nao asijue kwamba wapo ambao hawana upendo wa kweli, wakiachwa wanaanza kumkumbuka Tabu ambaye alikuwa halisi kwao.

Anaongeza: “Niliwahi kumkabidhi mtu mamilioni ya pesa nikiwa naye kwenye mahusiano ili afungue biashara, nilichokuja kufanyiwa nilimuachia Mungu, baada ya kupata pesa akawa anakula na wanawake wengine wakati lile ni jasho lake, ila mwisho wa siku akaishia kufeli maana pesa ya dhuluma siyo nzuri.

KAME 03

“Baada ya hapo nikajipa moyo wa kupambana tena, kwani siyo mlemavu, nimepewa akili na mikono miwili ya kupambana, nina uwezo wa kupata pesa ya kula, kwenda hospitali na kuisaidia jamii inayonizunguka, hilo kwangu ni bora zaidi.

“Ukiachana hilo kwenye maisha ya kazi wanashangaa Tabu anafanya vizuri kwa nini haonekani kwenye tamthilia, inakuwa ngumu wengi wao wana hofu kuona wakikupa sini fulani utawafunika na hawawezi wakakaa na wewe wakaelewa kipi ukikifanya kitakuwa bora, wanakupanga kwenye sini wakati mwingine ili mradi, kumbe mtu ni mstaarabu tu na ukafanya kazi yao kwa ubora, ila wanaona bora wakudidimize.”

“Jambo lingine wasanii tunakosa unaweza ukampigia msanii mkubwa anakwambia hana nauli, ila kwenye TV anaonekana tajiri sisi tunajuana, kwenye tv tunajimwambafai tu wakati hatuna uwezo, ingawa kwa upande wangu nikiwa sina sina, nikiwa nacho ninacho, kuna wakati unaweza ukakosa hadi kodi, ila ukawapigia watu unaofanya nao kazi wakakupa pesa.”

KAME 04

Anasema kitu kinachomsaidia aendelee kuwa imara ana ushikaji na wanaume ambao anaona wamenyooka, tofauti na wanawake ambao wamejaa masengenyo: “Wanawake nikifanya nao kazi inaishia nao eneo la kazi, unacheka unamaliza hapo hapo, tofauti na wanaume hawana maneno ya kupindapinda, hilo limenisaidia zaidi kuwa imara, naepukana na mambo mengi ya urafiki ya watoto wa kike, uongo, wivu, tamaa vimewajaa, ukimposti mpenzi wako atataka kuleta chokochoko ili muachane, au umempa siri zako unaanza kuwa na wasiwasi, kiukweli kutokuwa na urafiki nao imenifanya niwe na amani.”

Jambo lingine analoona linagharimu maisha ya mastaa wengi wanaleta ujuaji katika mahusiano: “Acha nijichane hata mimi mwenyewe, unapokutana na mtu maisha ya ustaa yawe na mipaka, lazima ufanane na uliye naye na siyo kumpanda kichwani, lazima atatafuta pa kupoa, wanaume wengi hawapendi kelele, hiyo ndiyo maana watu wanaolewa kesho wanaachika, tujifunze nidhamu.”