Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

West Ham yavunja rekodi ya usajili Championship

WEST HAM Pict

Muktasari:

  • Engels, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji, amesaini mkataba wa miaka mitano na West Ham, ambao msimu huu utashiriki Championship baada ya kushuka daraja kutoka Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: WEST HAM United imeweka rekodi mpya ya usajili katika ligi za EFL baada ya kumsajili kiungo Arne Engels kutoka Celtic kwa ada ya pauni milioni 22.

Engels, 22, ambaye ni raia wa Ubelgiji, amesaini mkataba wa miaka mitano na West Ham, ambao msimu huu utashiriki Championship baada ya kushuka daraja kutoka Ligi Kuu England.

Ada hiyo imevunja rekodi ya usajili wa klabu inayoshiriki Championship, iliyokuwa inashikiliwa na Ipswich Town baada ya kutumia pauni milioni 17.5 kumsajili mshambuliaji wa Norway, Sindre Walle Egeli, mwaka mmoja uliopita.

West Ham ilishuka daraja Mei na sasa inaanza msimu wake wa kwanza Championship tangu mwaka 2012 kwa kucheza ugenini dhidi ya Burnley Jumapili.

Hata hivyo, Engels hatakuwa tayari kucheza mchezo huo wa kwanza, hivyo anatarajiwa kuanza maisha yake West Ham katika mchezo wa ligi dhidi ya Charlton Athletic utakaopigwa London Stadium, Jumamosi Agosti 22.

Engels alicheza mechi 100 akiwa na Celtic baada ya kujiunga na mabingwa hao wa Scotland akitokea Augsburg mwaka 2024, akifunga mabao 17 na kutoa asisti 22.

Akiwa Celtic, alifanikiwa kutwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu Scotland, baada ya kuanza maisha yake ya soka katika akademi ya Club Brugge.

Usajili wa Engels ni wa nne kwa West Ham katika dirisha hili la usajili, baada ya kumchukua kiungo wa Venezuela, Keiber Lamadrid, beki wa Uholanzi, Joel Veltman, na winga wa Israel, Manor Solomon.

Mkurugenzi wa usajili wa wachezaji wa West Ham, Nils Koppen, amesema Engels amekuwa akifuatiliwa na klabu hiyo kwa muda mrefu.

“Arne ni mchezaji ambaye tumekuwa tukimfuatilia kwa muda na amekuwa miongoni mwa malengo yetu muhimu.

“Bado ni kijana na ana miaka yake bora mbele yake, lakini tayari ana uzoefu mkubwa na amejiimarisha katika klabu kubwa, akionyesha uthabiti na kujiamini,” amesema Koppen.

Ameongeza kuwa Engels ana sifa zinazomfanya aendane na mipango ya klabu hiyo.

“Arne ana sifa zinazofaa, ndani na nje ya uwanja, kuendana na kile tunachojenga kuelekea siku zijazo. Ana hamasa kubwa ya kuwa hapa na kukabiliana na changamoto hii.”

Engels, ambaye amecheza mechi nne na timu ya taifa ya Ubelgiji, amesema lengo lake kubwa ni kuisaidia West Ham kurejea Ligi Kuu England.

“Ni mradi mzuri sana kuwa sehemu yake. Lengo kubwa ni kujaribu kurejea Ligi Kuu. Hilo ndilo lengo letu.

“Ni jukumu langu kusaidia timu kufikia hilo na kwa kushirikiana na mashabiki kupata ushindi. Natumaini utakuwa msimu mzuri,” amesema.