Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PESA INAONGEA! Uhamisho 10 ghali zaidi kuwahi kutokea kama ungefanyika leo na gharama zake

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Rio Ferdinand aliweka rekodi mbili za uhamisho wa England katika maisha yake ya soka. Kwanza ilikuwa alipohamia Leeds United akitokea West Ham United mwezi Novemba 2000 kwa ada ya Pauni 18 milioni, lakini uhamisho wake wa pili kwenda Manchester United akitokea Leeds Julai 2002 kwa Pauni 29 milioni uliivunja tena rekodi hiyo.

LONDON, ENGLAND: ADA za uhamisho wa wachezaji zimepanda kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa fedha kwenye mchezo wa soka, jambo lililosababisha bei za wachezaji kupanda kwa kasi. Hapa, Daily Star Sport inaangalia uhamisho 10 ghali zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka, kama ungekuwa unafanyika leo.

Rio Ferdinand aliweka rekodi mbili za uhamisho wa England katika maisha yake ya soka. Kwanza ilikuwa alipohamia Leeds United akitokea West Ham United mwezi Novemba 2000 kwa ada ya Pauni 18 milioni, lakini uhamisho wake wa pili kwenda Manchester United akitokea Leeds Julai 2002 kwa Pauni 29 milioni uliivunja tena rekodi hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti wa ValuBall, ambao umezingatia mfumuko wa bei na marekebisho ya thamani ya ada, uhamisho huo ungekuwa na thamani ya Pauni 174.8 milioni katika soko la sasa.

USAJ 03

Ferdinand anaingia katika nafasi ya 10 kwenye orodha hiyo, huku nafasi ya tisa ikishikiliwa na nyota mwingine wa zamani wa England, Stan Collymore, ambaye alihama kutoka Nottingham Forest kwenda Liverpool 1995/96 kwa Pauni 8.5  milioni. Leo, uhamisho huo ungekuwa na thamani ya Pauni 179.3 milioni.

Gareth Bale alivunja rekodi ya dunia ya uhamisho 2013 alipohamia Real Madrid kutoka Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni 85.1 milioni. Hata hivyo, kama dili hilo lingefanyika leo, Tottenham ingekuwa na kiasi kinacholingana na Pauni 92.3 milioni za kutumia kusajili wachezaji mbadala kadhaa waliokuja baada ya kuondoka kwake.

Marc Overmars alifurahia miaka mitatu ya mafanikio makubwa akiwa Arsenal kabla ya kuhamia Barcelona 2000 kwa Pauni 25 milioni, kiasi ambacho kingelingana na Pauni 196 milioni katika soko la sasa.

Huo hauwezi kuwa miongoni mwa matumizi mabaya zaidi ya fedha yaliyowahi kufanywa na miamba hiyo ya Catalunya, licha ya Overmars kushindwa kuonyesha kiwango chake cha Arsenal kutokana na matatizo ya majeraha, kwa sababu mchezaji aliyefanya hilo anakuja baadaye.

USAJ 01

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza jinsi maisha na kazi ya soka ya Paul Gascoigne ‘Gaza’ yangekuwaje kama angecheza chini ya Sir Alex Ferguson katika kikosi cha Manchester United. Lakini, Lazio ilipolipa Pauni 5.5 milioni kumsajili nyota huyo wa England 1992, swali linaweza kuwa zaidi kama United ingeweza kumudu ada hiyo, ambayo leo ingekuwa na thamani ya Pauni 196.9 milioni.

Saga ya uhamisho wa Philippe Coutinho kutoka Liverpool kwenda Barcelona ilifikia mwisho Januari 2017, ambapo klabu hiyo ya Camp Nou ililipa Pauni 142 milioni ambazo leo zingekuwa sawa na Pauni 217 milioni, kwa mchezaji ambaye baadaye alionekana kuwa usajili wa kukatisha tamaa.

Mchezaji huyo wa Brazil alianza vizuri, lakini pigo kubwa zaidi lilikuja alipofunga mabao mawili dhidi ya Barcelona akiwa kwa mkopo Bayern Munich katika ushindi wa mabao 8-2, baada ya kuondolewa kwenye mipango ya timu hiyo miezi 18 tu baada ya kusajiliwa.

USAJ 05

Nicolas Anelka ni mchezaji anayefahamu sana masuala ya uhamisho, lakini kuhama kwake kutoka Arsenal kwenda Real Madrid 1999 kwa Pauni  23.5 milioni kulionyesha thamani ya kipaji na uwezo wake.

Ingawa mambo hayakumuendea vizuri katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, ada hiyo ambayo leo ingekuwa na thamani ya Pauni 225.5 milioni ilikuwa na faida kubwa kwa Arsenal.

Alan Shearer alivunja rekodi ya dunia ya uhamisho 1996 alipohamia Newcastle United akitokea Blackburn Rovers kwa Pauni 15 milioni, ambapo nyota huyo wa kimataifa wa England alirejea nyumbani St James’ Park katika uhamisho ambao leo ungekuwa na thamani ya Pauni 238 milioni.

USAJ 04

Eden Hazard aliondoka Chelsea 2019 na kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa Pauni 150 milioni ambao ulitarajiwa kumfanya Mbelgiji huyo aendelee kuonyesha kiwango chake bora katika klabu kubwa zaidi duniani.

Hata hivyo, dili hilo ambalo leo lingekuwa na thamani ya Pauni 245.3 milioni liligeuka kuwa janga, na miaka minne baadaye alistaafu akiwa amefunga mabao saba pekee katika mechi 76.

Anayeongoza orodha hiyo ni Cristiano Ronaldo, ambaye huenda ndiye mchezaji mwenye uhamisho muhimu zaidi kuwahi kutokea, ambapo alijiunga na Real Madrid 2009 kwa ada ya Pauni 80 milioni, uhamisho ambao uliweka msingi wa ada kubwa zilizokuja baadaye.

USAJ 02

Ingawa rekodi hiyo ilivunjwa 2013 na Bale kwenda Real Madrid kwa Pauni 85.1 milioni na 2016 na Paul Pogba kujiunga na Manchester United kwa Pauni 89 milioni, thamani za uhamisho hazikupanda kwa kasi hadi Neymar alipojiunga na Paris Saint-Germain 2017 kwa Pauni 200 milioni na kubadilisha kabisa soko.

Kama uhamisho wa Ronaldo ungekuwa unafanyika leo, ungekuwa na thamani inayokadiriwa ya Pauni 291.6 milioni.

Na sasa fikiria jinsi mashabiki wa Manchester United wangeitikia kama wangekuwa na kiasi hicho cha fedha, lakini wakasajili Antonio Valencia kutoka Wigan, Gabriel Obertan ambaye hakujulikana sana, pamoja na Michael Owen aliyekuja bure kama ilivyokuwa wakati huo.