Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penzi la David Raya, Tatiana katika ardhi ya Tanzania

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Tatiana, kutoka kuwa mpenzi aliyekuwa akimsapoti Raya katika safari yake ya soka, kwa sasa ni mke na mama wa mtoto mmoja, huku wakiendelea kujenga familia yao na kushirikisha baadhi ya nyakati muhimu za maisha.

Kipa wa Arsenal na timu ya taifa ya Hispania, David Raya, 30, amekuwa katika ndoa na Tatiana Trouboul, 27, tangu mwaka uliopita, ndoa ambayo kwao imebeba kumbukumbu nzuri kuhusu Tanzania.

Tatiana, kutoka kuwa mpenzi aliyekuwa akimsapoti Raya katika safari yake ya soka, kwa sasa ni mke na mama wa mtoto mmoja, huku wakiendelea kujenga familia yao na kushirikisha baadhi ya nyakati muhimu za maisha.

Tangu mwaka 2021, uhusiano wao umepitia hatua mbalimbali, kuanzia uchumba, ndoa, fungate nchini Tanzania hadi kupata mtoto wao wa kwanza.

Tatiana kutokea Barcelona, Hispania, yeye ni mwanamitindo ambaye pia amejikita katika ujasiriamali, kwa sasa anaishi London, ambako amekuwa akionyesha sehemu ya maisha yake ya kifahari katika mitandao ya kijamii.

Mwanzilishi huyo wa chapa ya mavazi iitwayo Weartrouboul, kabla ya kupata umaarufu katika mitandao pamoja na uhusiano wake na Raya, taarifa mbalimbali zinadai aliwahi kufanya kazi katika klabu ya usiku.

Katika ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi zaidi ya 36,600, mara kwa mara amekuwa akiposti video na picha zinazoonyesha mtindo wake wa maisha ulivyo kuanzia nyumbani kwao hadi unapoenda ufukweni kupunga upepo.

Kwa jumla Tatiana na Raya wanaonekana ni wapenzi wanaopenda kuishi maisha ya kifahari na ndio sababu hasa wamekuwa wakisafiri kwenda maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kwa ajili ya mapumziko.

Wawili hao walianza uhusiano mwaka 2021, wakati huo Raya bado alikuwa akiichezea Brentford kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Arsenal na alikuja kusajiliwa rasmi na kuwa nguzo muhimu akiisaidia klabu hiyo kutwaa taji la EPL msimu uliopita.

Hata hivyo, wawili hao hawakuweka wazi penzi lao mara moja, uhusiano wao ulianza kufahamika zaidi hadharani mwaka 2022, ikiwa ni baada ya kuanza kuonekana pamoja na kuposti picha zao kwenye mitandao ya kijamii.

Tangu wakati huo, Raya na Tatiana wamekuwa wakionekana pamoja katika maeneo mbalimbali, hasa wakati wa mapumziko baada ya msimu wa ligi kumalizika.

Wakati wa michuano ya Euro 2024 nchini Ujerumani, Tatiana alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimpa sapoti kipa huyo wa Hispania, ambao walibeba taji hilo kwa kuifunga England.

Vilevile katika Kombe la Dunia 2026 na Hispania waliibuka mabingwa mbele ya Argentina, Tatiana alikuwepo pamoja na Raya ingawa golikipa huyo hakupata nafasi ya kucheza mechi yoyote.

Wawili hao walipiga picha ya pamoja katika uwanja wa MetLife wakiwa wameshikilia kombe hilo lenye hadhi ya juu zaidi dniani.

Hatimaye Julai 5, 2025, Raya na Tatiana walifunga ndoa na kufanya sherehe ya faragha iliyohudhuriwa na watu wachache huko Hispania. Sherehe hiyo ilifanyika kwa usiri mkubwa huku marafiki wa karibu pekee wakialikwa. Mbali na wanafamilia, baadhi ya wachezaji wenzake Raya, akiwemo Kai Havertz na Mikel Merino, pia walialikwa kwenye harusi hiyo ambayo baadaye picha zake ziliwekwa katika mitandao.

Oktoba 5, 2025, wawili hao walitangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Raya aliposti picha Instagram ikimwonyesha Tatiana akiwa ameshika tumbo lake huku mchezaji huyo akiweka mkono wake juu yake.

Katika maelezo ya picha hiyo, Raya aliandika; Ninakuahidi kwamba daima nitakulinda na kukujali. Mashabiki pamoja na wachezaji wenzake mbalimbali walimpongeza kwa hatua hiyo.

Tangazo hilo lilikuja siku moja baada ya Raya kucheza mechi ya ligi dhidi ya West Ham United ambapo Arsenal iliibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Kwa jumla habari hiyo njema ilikuja takribani miezi mitatu baada ya wawili hao kufunga ndoa, ambapo baada ya harusi walisafiri kuja Tanzania kwa ajili ya fungate yao.

Wakiwa Tanzania walifanya utalii wakitembelea fukwe, kwenda mbugani kutazama wanyamapori pamoja na kufurahia utamaduni uliomkosha Raya ambaye alikuja kuposti video akizungumza lugha ya Kiswahili.

Kwa sasa, Tatiana anaendelea kujenga jina lake katika ulimwengu wa mitindo na mitandao ya kijamii, huku Raya akiendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arsenal.

Ikumbukwe Raya alijiunga rasmi na Arsenal baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja. Julai 2024, ndipo ilitangazwa Raya amejiunga na klabu hiyo moja kwa moja.

“Baada ya mwaka mmoja wa mkopo, hatimaye naweza kusema kuwa mimi ni mchezaji wa Arsenal kwa miaka ijayo. Ni ndoto iliyotimia kuwa hapa na ninataka kuwashukuru kwa sapoti yote ambayo tayari mmenipa kwa kipindi kilichopita,” alisema David Raya.