Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenger kawajaza England, kisha kawakataa

Muktasari:

  • England ilitarajia kufahamu wapinzani wao watakaokwenda kukabiliana nao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada katika droo ya makundi iliyotarajia kufanyika Ijumaa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA, Arsene Wenger amesema England inaweza kushinda Kombe la Dunia, lakini amekiri kikosi cha Three Lions haina ubora kama Ufaransa.

England ilitarajia kufahamu wapinzani wao watakaokwenda kukabiliana nao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada katika droo ya makundi iliyotarajia kufanyika Ijumaa.

Kocha wa zamani wa Arsenal, Wenger, ambaye kwa sasa ni bosi wa maendeleo ya soka wa FIFA, alisema: “England ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa kwenye Kombe la Dunia. Siku zote wamekuwa wakifanya vizuri, wamepiga hatua kubwa. Wana viwango vya kushinda.

“Lakini, kama tukibaki kama ilivyo, nadhani Ufaransa inapewa nafasi kubwa. Kwa sababu moja tu. Ina washambuliaji wa viwango vya dunia kuliko nchi nyingine yoyote ile. Kuwa na benchi la aina hiyo na viwango vya ubora huo unakufanya kuwa tofauti.”

Kwenye kikosi cha Ufaransa kuna mastraika wa moto kabisa kama Kylian Mbappe, Hugo Ekitike, Ousmane Dembele, Desire Doue, Marcus Thuram na Randal Kolo Muani, itakuwa moja ya timu zitakazobeba makundi sambamba na England, hivyo nchi hizo mbili zinaweza zisikutane hadi fainali.

Kocha wa England, Thomas Tuchel alitua Marekani, Alhamisi kwa ajili ya kushuhudia upangaji wa makundi ya fainali hizo za Kombe la Dunia 2026. Kikosi cha England, Three Lions kilishinda mechi zake zote nane bila ya kuruhusu bao katika mechi za kufuzu michuano hiyo na mkurugenzi mtendaji wa FA, Mark Bullingham alisema: “Thomas amekuja na hakika amefanya kazi nzuri sana. Ameleta nguvu kubwa sana kambini na unaweza kuona jinsi wachezaji wanavyokubaliana naye. Tunasubiri kwa hamu fainali hizo.”

Wenger, alibainisha pia na kudai anadhani timu zimejifunza mengi kuhusu hali ya joto ilivyo kama ilivyotokea kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.