Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bounemouth yakataa ofa nono ya Chelsea

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Viongozi wa Bournemouth wameiambia Chelsea wazi kuwa hawatakaribisha ofa nyingine yoyote, wakisisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza mmoja wa wachezaji wao muhimu katika dirisha hili la usajili.

Bournemouth imekataa ofa ya pauni 64 milioni iliyowasilishwa na Chelsea kwa ajili ya kumsajili kiungo Alex Scott.

Viongozi wa Bournemouth wameiambia Chelsea wazi kuwa hawatakaribisha ofa nyingine yoyote, wakisisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza mmoja wa wachezaji wao muhimu katika dirisha hili la usajili.

Hata hivyo, hali inaendelea kuwa ngumu kwa Bournemouth baada ya Scott, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, kukataa kusaini mkataba mpya ambao umekuwa mezani kwa takribani miezi miwili.

Mbali na Chelsea, klabu za Arsenal, Manchester United, Tottenham Hotspur na Manchester City pia zilionyesha nia ya kumsajili Scott mapema katika dirisha hili la usajili.

Mnamo Juni, BBC Sport iliripoti Bournemouth ilikataa pia maombi ya Arsenal ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22.

Scott alijiunga na Bournemouth mwaka 2023 akitokea Bristol City kwa ada ya pauni milioni 25, na kwa sasa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake.

Licha ya kukataa kusaini mkataba mpya, Bournemouth imesisitiza hadharani, kwa mchezaji mwenyewe na kwa klabu zinazomtaka, kuwa Alex Scott ataendelea kubaki katika klabu hiyo msimu ujao.


Sam Nombe

ROTHERHAM United iko tayari kumuuza mshambuliaji Sam Nombe (27), lakini ni iwapo klabu itapata dau inalolitaka. Tayari imekataa ofa kadhaa kutoka MK Dons, huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi.


John Souttar

CARDIFF City, Sheffield United na Watford zinaendelea kumuwania beki wa Rangers, John Souttar (29). Rangers inahitaji ada ya mamilioni ya pauni, huku mchezaji huyo akionekana kutokuwa tayari kujiunga na Leicester City kutokana na kutotaka kucheza League One msimu ujao.


Mikael Mandron

MSHAMBULIAJI Mikael Mandron atajiunga na Stevenage kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka St Mirren. Uhamisho wake wa kwenda Oxford United ulivunjika kutokana na zuio la usajili lililoikumba klabu hiyo, hivyo Stevenage ikatumia nafasi hiyo kumshawishi nyota huyo.


Ben Nelson

WEST Ham United inafikiria kumsajili beki wa Leicester City, Ben Nelson (22), kwa ada nafuu baada ya Leicester kushuka hadi League One. Kocha wa West Ham anaamini beki huyo ana uwezo mkubwa wa kuendelea kuimarika akiwa ndani ya Ligi Kuu England.


Daizen Maeda

IPSWICH Town imefikia makubaliano ya awali na Celtic ya kumsajili mshambuliaji wa Japan, Daizen Maeda (28), kwa ada ya pauni milioni nane pamoja na nyongeza ya pauni milioni mbili. Sasa pande zote zinakamilisha taratibu za mwisho kabla ya kutangaza uhamisho huo rasmi.


Carlos Baleba

MANCHESTER United bado inahitaji kiungo wa kati, lakini imepunguza kasi katika harakati za kuwafuata Carlos Baleba wa Brighton na Alex Scott wa Bournemouth, wote wenye miaka 22. Sababu kubwa ni gharama kubwa za usajili zinazotajwa kuzidi bajeti iliyotengwa na klabu hiyo.


Marcus Rashford

VIGOGO wa Ligi Kuu England, Tottenham Hotspur, Chelsea na Arsenal, wanapanga kumwania mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford (28). Nyota huyo wa England anaendelea kuvutia klabu kadhaa baada ya hatma yake Old Trafford kuwa na sintofahamu, huku mazungumzo yakitarajiwa kushika kasi kabla dirisha la usajili halijafungwa.


Emiliano Martinez

KIPA wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez (33), anawindwa na Juventus, huku Arsenal ikiendelea kumfuatilia beki wa Villa na England, Ezri Konsa (28). Klabu zote mbili zinatazamiwa kuwasilisha hatua rasmi ikiwa mazungumzo yataendelea vizuri katika siku zijazo.


Ousmane Diomande

NOTTINGHAM Forest ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kumsajili beki wa Sporting CP na timu ya taifa ya Ivory Coast, Ousmane Diomande (22). Klabu hiyo ina matumaini ya kukamilisha uhamisho huo haraka ili mchezaji huyo aanze maandalizi ya msimu mpya pamoja na kikosi.