Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenger: Arsenal? Inategemea kona tu

WENGER Pict

Muktasari:

  • Man United ilipata ushindi wa kushtua nyumbani kwa Arsenal, ikiwa ni siku nane baada ya kutoka kuwafunga Manchester City, ikiwa ni mwendelezo wa mwanzo mzuri wa kocha wa muda Michael Carrick.

LONDON, ENGLAND: ARSENE Wenger amekiri Arsenal inategemea sana mipira ya kona huku akibainisha mabeki wao walikuwa kwenye hofu na wasiwasi mkubwa wakati wa kipigo cha mabao 3-2 mbele ya Manchester United, uwanjani Emirates.

Man United ilipata ushindi wa kushtua nyumbani kwa Arsenal, ikiwa ni siku nane baada ya kutoka kuwafunga Manchester City, ikiwa ni mwendelezo wa mwanzo mzuri wa kocha wa muda Michael Carrick.

Carrick alishuhudia kikosi chake kikitokea nyuma baada ya Arsenal kutangulia kufunga, ikasawazisha na kufunga jingine kisha vijana wa Mikel Arteta kusawazisha kabla ya kuchapwa bao la tatu ambalo lilikuwa la mwisho kwenye mechi hiyo.

Shuti la mbali la Matheus Cunha lililoamua mchezo huo wa mabao matano, huku Wenger akimpongeza Carrick kwa kazi nzuri aliyofanya tangu aajiriwe, baada ya kuona mabadiliko chanya chini ya kocha huyo wa zamani wa Middlesbrough.

WENG 02

Akizungumza kuhusu timu yake ya zamani, Wenger alipendekeza michezo yao mara nyingi huamuliwa kwa ‘mapambano kwenye mipira ya kona’, huku The Gunners wakitegemea sana mipira ya adhabu, jambo lililowasaidia kupata bao lao la pili. Mfaransa huyo pia alibaini upande mpya katika uchezaji wa mabeki wao wa kati wa vijana hao wanaonolewa na Mhispaniola, Arteta.

Wenger amesema kwenye BeIN Sports: “Unapofungwa mabao matatu nyumbani ni vigumu kushinda. Mabao yaliyofungwa na pande zote mbili yalionyesha kwa kiasi fulani namna timu hizo mbili zilivyocheza. Manchester United imejengwa vizuri, kuna mshikamano mzuri, lakini Arsenal ilikuwa zaidi imeamuliwa na nguvu na mapambano kwenye mipira ya kona, kwa mfano bao la pili. Bao la kwanza pia halikutokana na uchezaji safi. Arsenal walijitahidi sana lakini walikosea kidogo, kama nilivyosema kipindi cha kwanza, subira na mshikamano wa kiufundi.”

Wenger aliongeza: “Ninaamini Carrick amepata mfumo mzuri unaotoa uwiano mzuri kati ya uimara wa ulinzi na kiwango kizuri cha kiufundi. Ni mara ya kwanza nilihisi mabeki wa kati wa Arsenal walikuwa na wasiwasi zaidi na hawakuwa imara kama walivyozoeleka katika mechi.”

WENG 01

Ushindi huo kwa Man United umefanya mbio za ubingwa kufunguka zaidi, huku ushindi wa Man City, Jumamosi ukiwaacha pointi nne tu nyuma. Hali hiyo ipo kwa Aston Villa waliopo nafasi ya tatu, baada ya kushinda ugenini dhidi ya Newcastle United, Jumapili. Arsenal imekusanya pointi mbili tu katika mechi zao tatu za mwisho, jambo lililoruhusu pengo kupungua.

“Bado wako mbele kwa pointi nne, lakini bado kuna maswali kuhusu uimara wa kisaikolojia wa timu,” amesema nahodha wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, kwenye Sky Sports huku Arsenal kwenye mechi zao zilizobaki, kipo pia kipute cha kuwakabili Man City.