Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Offside ya Arsene Wenger imeiva!

WENGER Pict

Muktasari:

  • Mara nyingi, sheria ya offside imekuwa ikiwavuruga mashabiki wengi wa soka. Lakini, sasa, aliyekuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuondoa utata huo.

ZURICH, USWISI: ILE ni offside. Mmefunga bao la offside. Ni mjadala ambao umekuwa ukiibuka mara kwa mara kutoka kwa mashabiki pindi timu zao zinapocheza na kutokea tukio la bao lililofungwa kuwa na utata kwa maana ya kuwapo na tukio la mchezaji kuotea (offside).

Mara nyingi, sheria ya offside imekuwa ikiwavuruga mashabiki wengi wa soka. Lakini, sasa, aliyekuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuondoa utata huo.

Mpango mpya wa mapinduzi ya sheria ya kuotea uliwekwa mezani na Wenger na sasa unakaribia kuchukua hatua muhimu zaidi baada ya FIFA na rais wake, Gianni Infantino kujiandaa kuwasilisha pendekezo la mabadiliko ya sheria hiyo huko IFAB.

Wenger amekuwa akisisitiza kwa muda mrefu mabadiliko makubwa ya sheria ya kuotea, akipendekeza kuwa mchezaji mshambuliaji ahesabiwe kuwa ameotea tu ikiwa mwili wake mzima uko mbele kabisa ya beki wa mwisho.

WENG 04
WENG 04

Mpango wa Wenger unakaribia kuidhinishwa

Mkutano wa kila mwaka wa IFAB unatarajiwa kufanyika Januari 20 jijini London, ambapo mapendekezo ya Wenger yatajadiliwa kwa kina, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la AS.

Pendekezo hilo pia litajadiliwa katika Mkutano Mkuu utakaofanyika Wales mwezi Februari. Wenger, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka Duniani wa FIFA, anataka mabadiliko makubwa ya sheria ya kuotea ambayo yatawanufaisha washambuliaji, kwani itamaanisha mchezaji hajaotea (onside) ikiwa sehemu yoyote ya mwili wake iko sambamba na beki wa mwisho wa ulinzi.

Wenger alieleza pendekezo hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2020, akisema: “Bado kuna nafasi ya kubadilisha sheria na kutoamua kuwa pua ya mchezaji imeotea kwa sentimita chache, kwa sababu unaweza kufunga kwa sehemu hiyo ya mwili. Badala yake, hutakuwa umeotea ikiwa sehemu yoyote ya mwili inayoruhusiwa kufunga iko sambamba na beki wa mwisho, hata kama sehemu nyingine ya mwili wako iko mbele. Hii itaondoa maamuzi ya milimita na tofauti ndogo sana.”

WENG 02

Kwanini Wenger anataka kubadilisha sheria ya kuotea?

Wenger amezungumzia mara kadhaa sababu zinazomfanya atake mabadiliko haya. Anaamini washambuliaji wamekuwa wakiumizwa zaidi tangu kuanzishwa kwa VAR, jambo ambalo halijapokelewa vizuri na mashabiki. Wenger pia alikumbusha jinsi mabadiliko kama hayo yalivyofanywa baada ya Kombe la Dunia la 1990, ambalo lilikuwa na wastani mdogo zaidi wa mabao katika historia.

“Baada ya Kombe la Dunia 1990 nchini Italia, kulikuwa na mabao machache sana,”  Wenger aliambia Bein Sports na kuongeza:

“Tuliamua kuwa hakuna kuotea tena ikiwa mko kwenye mstari mmoja na beki. Katika hali ya shaka, shaka inamnufaisha mshambuliaji. Lakini kwa VAR, faida hii imepotea na kwa watu wengi hilo linakatisha tamaa. Ndiyo maana nilipendekeza kuwa mradi tu sehemu yoyote ya mwili wako iko sambamba na beki, basi haujaotea. Tunajaribu hili sasa. Ndani ya mwaka mmoja, IFAB itafanya uamuzi, sio mimi.”

WENG 03

Rais wa FIFA atoa tamko

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ameashiria kuwa mpango wa Wenger unaweza kupewa kibali. Akizungumza kwenye Mkutano wa Michezo Duniani, alisema: “Tuchukulie mfano wa sheria ya kuotea, ambayo imekuwa ikibadilika kwa miaka mingi. Labda katika siku zijazo, mshambuliaji atalazimika kuwa mbele kabisa ya beki ili ahesabiwe kuotea.”

Majaribio tayari yamefanyika. Msemaji wa FIFA aliliambia gazeti la The Times mwaka 2024:

“Mjadala kuhusu kubadilisha sheria ya kuotea si mpya. Hatutarajii kuiona ikitumika kwenye ngazi za juu hivi karibuni. Wazo hili lilianza mwaka 2020 na tukaona ni muhimu kulijaribu kuona athari zake kwenye mchezo. FIFA ilijitolea kufanya majaribio ya sheria mpya inayomnufaisha mshambuliaji, ambayo imetumika kwenye mashindano ya vijana barani Ulaya. Tutaendelea na majaribio haya na kutathmini matokeo.”

WENG 01

Kuna watu wanamkosoa Wenger

Mpango huo umekosolewa na aliyekuwa beki wa Liverpool, Jamie Carragher. Aliandika kwenye X: “Hili litakuwa baya kwa mchezo kwa sababu timu zitalazimika kujilinda kwa njia tofauti kabisa na tunavyoona sasa. Kutakuwa na ulinzi wa chini (low block) na timu zitakuwa za kujihami zaidi.”


Nini kinafuata?

Mpango wa Wenger umeibua mjadala mkubwa na sasa utakaguliwa kwa kina katika miezi ijayo. Mawazo ya sasa yanaonyesha kuwa kama utaidhinishwa mabadiliko hayo yanaweza kuanza kutumika msimu wa 2026-27.