Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia wajiapiza kwa Salah, Vinicius Jr

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Salah, amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na uhamisho kwenda Saudi Arabia, huku klabu kadhaa kubwa zikiwa tayari kumlipa mshahara mnono unaoweza kuvunja rekodi.

MABOSI wa Ligi Kuu Saudi Arabia wamewaweka Mohamed Salah, 33, wa Liverpool na Vinicius Jr, 25 wa Real Madrid katika orodha ya mastaa inaotaka kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa ni mpango wao wa kuinua hadhi ya ligi hiyo kimataifa.

Salah, amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na uhamisho kwenda Saudi Arabia, huku klabu kadhaa kubwa zikiwa tayari kumlipa mshahara mnono unaoweza kuvunja rekodi.

Vyanzo vya ndani kutoka nchi hiyo vinaamini Salah ataondoka Liverpool na kujiunga nao dirisha la majira ya kiangazi na ameshafanya uamuzi.

Vinicius Jr naye amekuwa akitajwa kutaka kusajiliwa na timu za ligi hiyo tangu mwaka juzi na hivi karibuni tetesi hizo zilipamba moto baada ya kuonekana hana uelewano mzuri na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo, Xabi Alonso.

Hata hivyo, Real Madrid haina nia ya kumuuza fundi huyu kwa sasa, lakini mabosi wa Saudia wako tayari kuwasilisha ofa ya kihistoria, ikiwemo ada kubwa ya uhamisho na mshahara wa mkubwa sana  ili kumshawishi mshambuliaji huyo ajiunge nao.


Guglielmo Vicario

INTER MILAN inamfuatilia kwa karibu kipa wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Italia, Guglielmo Vicario, 29, kama sehemu ya mpango wao wa kumtafuta mrithi wa kipa wao mkongwe, Yann Sommer, 37, ambaye huenda akandoka mwisho wa msimu huu.

Vicario amekuwa akionyesha kiwango bora tangu ajiunge na Tottenham na Inter wanamwona umri wake na uzoefu wa Serie A vinamfanya awe chaguo sahihi kwao.

Tottenham haina presha juu yake na haitaki kumwachia urahisi. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Jorgen Strand Larsen

CRYSTAL PALACE imefanya mazungumzo ya awali na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Norway, Jorgen Strand Larsen, 25, dirisha hili ikiwa ni kwenye juhudi zao za kuongeza makali kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Strand Larsen amekuwa akionyesha kiwango katika Ligi Kuu England, licha ya timu yake kuonekana haifanyi vizuri.

Palace inaamini staa huyu atasaidia sana kuongeza ubora katika safu yao ya ushambuliaji ambayo imekuwa na changamoto kadhaa tangu kuanza kwa msimu huu. Kwa sasa mazungumzo bado yapo katika hatua za awali.


Kobbie Mainoo

MANCHESTER UNITED ipo tayari kufungua rasmi mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo wao chipukizi wa timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, 20, ikiwa ni wiki kadhaa tangu aonekane kurudi katika kiwango cheke baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim ambaye aliweka wazi staa huyo anakosa baadhi ya vitu ambavyo yeye anavihitaji ndiyo maana amekuwa hamchezeshi kikosi cha kwanza.

Mkataba wa Mainoo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na awali alihusishwa sana na Napoli ambayo ilikuwa tayari kumsajili kwa mkopo wa nusu msimu ambao ungekuwa na kipengele cha kumsainisha mkataba wa kudumu.


Douglas Luiz

CHELSEA inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Brazil, Douglas Luiz, 27, kwa kipindi kilichobaki cha msimu huu.

Luiz kwa sasa yuko Nottingham Forest kwa mkopo akitokea Juventus, lakini amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza  cha timu hiyo hali iliyofanya Chelsea kupiga hodi na kuanza kuzungumza na wawakilishi wake.

Chelsea inataka kumsajili fundi huyu kwa ajili ya kuboresha eneo lao la kiungo ambalo wanaamini lina mapungufu kwa sasa. Mkataba wa Douglas na Juventus unamalizika mwaka 2029.


Harvey Elliott

Charlotte FC ya Ligi Kuu ya Marekani imeonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Harvey Elliott, 22.

Elliott, ambaye kwa sasa yuko Aston Villa kwa mkopo kutoka Liverpool, mkataba wake na majogoo hao wa Jiji la London unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu.

Charlotte FC inaamini ujio wa Elliott unaweza kuongeza ubunifu, kasi na mvuto wa kibiashara ndani ya kikosi chao. Hata hivyo, uamuzi wa mwisho utategemea na msimamo wa Liverpool pamoja na utayari wa mchezaji mwenyewe.


Josh Sargent

LEEDS UNITED na Sunderland hueda zikaangukia pua katika harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Norwich City na timu ya taifa ya Marekani, Josh Sargent, 25, dirisha hili.

Taarifa zinaeleza Sargent ana hamu kubwa ya kurejea Major League Soccer, huku Toronto FC ikitajwa kuwa chaguo lake kuu kwa sasa. Norwich City ipo kusikiliza ofa kutoka kwa timu zinazomhitaji.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza  mechi 24 za michuano yote.


Joshua Zirkzee

AS ROMA pamoja na klabu nyingine kadhaa Ulaya bado zipo kwenye mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24.

Kwa mujibu wa taarifa, Man United bado haijatoa uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo, lakini inaonekana kuwa tayari kumtoa kwa mkopo au hata uhamisho wa kudumu ikiwa itawasilishwa ofa itakayokidhi matarajio yao.

Mkataba wa sasa wa Zirkzee unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote na kufunga mabao mawili.