Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majibizano ya Mangungu, Magori tatizo ni hili!


UWEPO wa makundi mawili yenye mlengo tofauti pamoja na vita za ndani kwa ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Simba utakaofanyika 2027, ni sababu mbili ambazo zinaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa mgogoro unaoanza kufukuta klabuni hapo.


Baada ya ripoti za muda mrefu juu ya minyukano ya chinichini ya baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo, mambo yalianza kujianika kwa umma juzi na jana baada ya viongozi wawili wakubwa ndani ya klabu hiyo, Murtaza Mangungu na Crescentius Magori kuvimbiana hadharani.

Kutofautiana kwa wawili hao kulianzia baada ya Magori ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kutoa taarifa ya kupinga uamuzi wa Mangungu ambaye ni Makamu wake wa kuunda Bodi Mpya ya Wadhamini wa Klabu hiyo.

“Tunapenda kuwataarifu Wanachama wote wa Simba kuwa hicho kilichofanyika Bunju siku ya leo (Agosti 2, 2026) siyo kikao rasmi cha mkutano maalum wa Simba. Hivyo maamuzi yote yaliyotangazwa huko ni batili na kinyume cha Katiba ya Simba.

“Kwa mujibu wa Katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho 2026, ibara ya 23, Mkutano Mkuu maalum utaandaliwa na Mwenyekiti wa Klabu kwa kushirikiana na Bodi ya Wa-kurugenzi.

Hata hivyo ibara hiyo inasema kuwa ajenda za mkutano huo zitaandaliwa kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi kama unaandaliwa na Mwenyekiti.

“Hivyo kesho (Jumatatu) tarehe 3/8/2026 kutakuwa na kikao cha bodi kujadili agenda ya Mkutano Mkuu maalum wa Wanachama. Mtajulishwa siku maalum ya Mkutano huo,” ilisema taarifa ya Magori.

Hata hivyo, siku moja baada ya Magori kutoa taarifa hiyo, Mangungu katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Crown FM, alishangazwa na taarifa ya Magori akisema hakuwa na uhalali wa kuitoa.

“Mathalani, imeshajulikana kwamba kuna kikao cha Bodi leo (jana). Mimi nimeenda nje ya utaratibu na nimeenda kufanya mku-tano. Kulikuwa na haja gani yeye kukanusha kabla ya uamuzi wa bodi? Bodi ni yeye au wale wajumbe wanaounda bodi? Yeye alishauriana na nani kutoa hiyo notisi? Bodi maana yake sio mtu, ni chombo,” alisema Mangungu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, chanzo cha mgogoro huo ni makundi mawili yenye maslahi tofauti ndani ya klabu hiyo lakini pia uwepo wa safu zinazojipanga kwa uchaguzi wa Simba mwakani.

“Kuna kundi ambalo linaamini linasimamia maslahi ya wanachama na mashabiki na lingine limekuwa likipigania maslahi ya mwekezaji ambayo linaona kama yanaporwa. Hili jambo sio jepesi kama watu wanavyofikiria na linaweza kuleta mpasuko mkubwa sana kwenye klabu,” alisema mmoja wa viongozi waandamizi ndani ya Simba.

Makamu wa zamani wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange ‘Ka-buru’ alisema kuwa makundi hayo mawili ndio chanzo cha kinachotokea Simba.

“Ndani ya uongozi tunafahamu kwamba tuna pande mbili ambazo ndizo zinatengeneza uongozi. Nadhani kuna kukosekana kwa mawasiliano, masikilizano na maslahi ya pamoja. Kila upande nadhani una maslahi yake na wanashindwa kukubaliana wawe na maslahi ya pamoja. Shida ipo hapo na nadhani nichukue nafasi kuwashauri na kuwaasa kwamba wakae chini, hayo mambo yaishie ndani na waangalie maslahi ya Simba,” alisema Kaburu katika mahojiano yake na Bongo FM.


SULUHU NI HII

Kwa mujibu wa katiba ya Simba, inaonekana kuwa vipengele vingi ambavyo vinamhusu mwenyekiti wa Simba ni lazima ashauriane na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, hivyo ili Simba iweze kuachana na migogoro ya mara kwa mara ni lazima pande hizi mbili zilikubali kuwa kitu kimoja na kufanya kazi pamoja badala ya kila mmoja kuwa mkubwa kuliko mwingine.

Ibara ya 33: ambayo inaelezea kuhusu muundo wa madaraka inaonyesha kuwa wajumbe wa baraza la wadhamini watapendekezwa na mwenyekiti, lakini kwa kushauriana na Bodi ya Wa-kurugenzi ya timu hiyo.

Ibara ya 29 ya katiba hiyo inasema kuwa Simba Sports itafanya kazi chini ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Company Limited.

Hii ni mifano ya kuonyesha kuwa ili Simba iachane na migogoro ya mara kwa mara ni lazima matawi haya ambayo yanatambulika zaidi kwenye klabu hiyo, yawe kitu kimoja lakini yote yakiwa na nguvu kusikilizana na kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Jambo lingine, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa uchaguzi wa mwakani unawezekana kuwa unahusika na migogori hii inaweza kuwa ya kweli, lakini ni wakati wa viongozi wote kuweka maslahi ya Simba mbele badala ya kuwaza kuhusu cheo ili timu hiyo iweze kusonga mbele.