Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo apotezea dili la Napoli

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mainoo, ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya England, alikuwa akifikiria kuondoka kwa mkopo ili kupata  muda mwingi zaidi wa kucheza baada ya kocha Ruben Amorim kuonyesha kutokuwa na mpango wa kumtumia.

LICHA ya tetesi za awali kuhusu uwezekano wa kutolewa kwa mkopo kwenda Napoli, kiungo chipukizi wa Manchester United, Kobbie Mainoo, 20, anatarajiwa kubaki ndani ya kikosi cha mashetani hao wekundu baada ya kurudi kikosini na kuwa tegemeo kikosi cha kwanza tangu Michael Carrick ateuliwe kuwa kocha wa muda.

Mainoo, ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya England, alikuwa akifikiria kuondoka kwa mkopo ili kupata  muda mwingi zaidi wa kucheza baada ya kocha Ruben Amorim kuonyesha kutokuwa na mpango wa kumtumia.

Inaelezwa roho yake na mapenzi yake yapo katika kikosi cha Man United na hata hicho kipindi alichokuwa anataka kuondoka kwenda Napoli na baadhi ya timu nyingine zilizohusishwa naye alihitaji kusaini tu mkataba wa mkopo wa nusu msimu na sio moja kwa moja.

Inadaiwa pia mabosi wa Man United bado wana imani sana na fundi huyu na hiyo ndio ilikuwa sababu ya kukataa kumuuza hata wakati ambao hakuwa akipata nafasi ya kucheza.

Mkataba wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, alionyesha kiwango bora sana katika kikosi cha kwanza cha Man United katika mechi ya dabi dhidi ya Man City wikiendi iliyopita.


Gabriel Jesus

PALMEIRAS imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus, 28, ambaye amekuwa na panda shuka nyingi.

Jesus, ambaye ametoka kupona jeraha la muda mrefu, bado ana mkataba na Arsenal hadi mwaka 2027, lakini hali ya kutokuwa chaguo la kwanza kikosi cha kwanza cha washika mitutu hao inaonekana kumchosha na anatamani kuondoka.

Arsenal bado haijaanza mazungumzo na timu yoyote lakini inaelezwa ipo tayari kufanya majadiliano na timu yoyote itakayohitaji saini yake.


Noah Sadiki

MANCHESTER UNITED inaendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo wa Sunderland na timu ya taifa ya DR Congo, Noah Sadiki, 21. Kwa mujibu wa taarifa, Man United inafikiria kutumia kiungo wao wa kimataifa wa Uruguay, Manuel Ugarte ,24, kama sehemu ya ofa ili kuhakikisha inashinda vita ya kumpata staa huyu.

Sadiki ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na Sunderland katika Ligi Kuu England msimu huu akiwa mmoja wa viungo wenye takwimu nzuri katika ukabaji na kuharibu mashambulizi ya timu pinzani.


Lucas Paqueta

FLAMENGO bado inaendelea kuonyesha nia ya kumsajili kiungo wa West Ham United, Lucas Paqueta, 28, licha ya mazungumzo kati ya klabu hizo mbili kusimama tangu wiki iliyopita.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu West Ham, lakini inadaiwa kutaka Brazil ambako Flamengo imeonyesha nia ya kumsajili.

Moja kati ya sababu zinazotajwa kutaka kuondoka Ulaya ni kutaka kukaa karibu na familia yake. Hata hivyo, hadi sasa vigogo wa West Ham wamegoma kumuuza.


Quinten Timber

WEST HAM na Aston Villa zimepata pigo katika harakati zao za kumsajili kiungo wa Feyenoord, Quinten Timber, 24, baada ya Marseille kuharakisha mchakato na kuwasilisha ofa rasmi ya kuipata huduma ya nyota huyo wa Uholanzi.

Timber aliachwa nje ya kikosi cha kwanza cha Feyenoord kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita, hali iliyoongeza uvumi huenda tayari yupo karibu kuondoka. West Ham na Villa zilikuwa za kwanza kuhusishwa naye.


Ibrahim Konate

MAZUNGUMZO ya mkataba mpya kati ya wawakilishi wa Liverpool na wale wa beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Ibrahima Konat, 26, bado yanaendelea lakini hakuna dalili ya kufikia mwafaka hivi karibuni.

Konate, ambaye yuko kwenye msimu wake wa tano Anfield, anaamini anastahili kuwa miongoni mwa mabeki wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi Ligi Kuu England, kutokana na mchango wake mkubwa katika kikosi cha Arne Slot.


Jeremy Jacquet

CHELSEA imefikia makubaliano binafsi na beki kinda wa Rennes, Jeremy Jacquet, 20, ikiwa ni katika juhudi zao za kuendelea kujenga kikosi chenye wachezaji wenye umri mdogo.

Hata hivyo, kazi kubwa ili kukamilisha dili hilo ni kuishawishi Rennes kupunguza bei ambayo wameiweka kwa sasa. Inaelezwa Rennes inahitaji zaidi ya Pauni 30 milioni ili kumuuza kinda huyo.


Marcos Senesi

BOURNEMOUTH imepanga kusimama kidete dhidi ya ofa yoyote itakayowasilishwa mezani kwa ajili ya beki wao wa kimataifa wa Argentina, Marcos Senesi, 28, dirisha hili la usajili, licha ya mchezaji huyo kukataa ofa kadhaa za kuongeza mkataba wake unaomalizika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Senesi yupo katika rada za Juventus na Barcelona ambazo zinamhitaji ili kuimarisha safu zao za ulinzi.