Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Welbeck aanza kazi Chelsea, afanya mazoezi ya kwanza Hong Kong

WELBECK Pict

Muktasari:

  • Welbeck mwenye umri wa miaka 35 alikamilisha uhamisho wake kutoka Brighton & Hove Albion kwa ada inayoripotiwa kufikia Pauni milioni 5 (takribani Sh17.8 bilioni), kabla ya kuungana na wenzake kambini.

Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Danny Welbeck, ameanza rasmi maisha yake ndani ya kikosi hicho baada ya kufanya mazoezi yake ya kwanza nchini Hong Kong, ambako klabu hiyo ipo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Welbeck mwenye umri wa miaka 35 alikamilisha uhamisho wake kutoka Brighton & Hove Albion kwa ada inayoripotiwa kufikia Pauni milioni 5 (takribani Sh17.8 bilioni), kabla ya kuungana na wenzake kambini.

Katika mazoezi hayo ya kwanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Arsenal alionekana akifanya mazoezi pamoja na nyota wa Chelsea akiwemo Mykhailo Mudryk, Pedro Neto na Tosin Adarabioyo, huku akianza kuzoea mazingira ya klabu yake mpya.

Welbeck anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya safu ya ushambuliaji ya Chelsea chini ya kocha Xabi Alonso, ambaye ameonyesha dhamira ya kuchanganya vijana na wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chake.

Mbali na hilo, mshambuliaji huyo atakutana tena na kiungo mkongwe Jordan Henderson, ambaye naye amejiunga na Chelsea dirisha hili la usajili, jambo linaloongeza uzoefu ndani ya kikosi cha The Blues.

Welbeck ameweka saini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka Stamford Bridge hadi Juni 2028, akibeba matumaini ya kuendeleza kiwango kizuri alichoonyesha msimu uliopita, alipofunga mabao 13 akiwa na Brighton.