Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanachopaswa kufanya vigogo wa Big Six kwenye dirisha hili la Januari

Muktasari:

  • Timu ambazo zitakuwa tayari kufungulia pochi zitakuwa na nafasi nzuri ya kusajili wachezaji inaowataka. Kuna dili za maana za Januari zilifanyika miaka ya hivi karibuni  – ikiwamo wa Martin Odegaard kwenda Arsenal, Luis Diaz kwenda Liverpool na Bruno Fernandes kwenda Manchester United miongoni mwao.

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la usajili wa wachezaji la Januari limefunguliwa na kuzipa klabu za Ligi Kuu England fursa ya kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya duru la pili la msimu. Kwa kawaida, usajili wa dirisha la katikati ya msimu litazifanya timu kuwa kwenye wakati mgumu kwani mara nyingi haipati wachezaji wenye viwango vinavyoshabihiana na pesa wanazouzwa sokoni.

Timu ambazo zitakuwa tayari kufungulia pochi zitakuwa na nafasi nzuri ya kusajili wachezaji inaowataka. Kuna dili za maana za Januari zilifanyika miaka ya hivi karibuni  – ikiwamo wa Martin Odegaard kwenda Arsenal, Luis Diaz kwenda Liverpool na Bruno Fernandes kwenda Manchester United miongoni mwao.

Lakini, kuna timu pia ziliingia mkenge kwenye usajili huo wa dirisha la Januari, waulize Chelsea, ambao walitoa Pauni 88.5 milioni kumsajili Mykhailo Mudryk kwenye dirisha la Januari 2023.

Kutokana na hilo, haya hapa matatizo makubwa kabisa ambayo klabu za Big Six zinapaswa kutafuta ufumbuzi wake kwenye dirisha hili la Januari.


Arsenal

Kikosi cha Arsenal kinaonekana kuandamwa na matatizo mengi ya maumivu ya misuli, akiwamo staa wao Bukayo Saka na tangu wakati huo miamba hiyo ya kocha Mikel Arteta imekuwa haina kiwango cha kufurahisha sana ndani ya uwanja. Arsenal sasa inapata shida kwenye kutengeneza nafasi za kutosha za mashambulizi. Kutokana na hilo, Arsenal inahitaji kumaliza tatizo hilo kwa kutafuta saluhu na ndiyo maana miamba hiyo ya Emirates imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams. Kocha Arteta pia anafikiria kumtema Marquinhos kwenye dirisha hili, huku klabu ikifikiria pia kutengeneza pesa kutoka kwa Al-Ittihad kutokana na kwamba timu hiyo ya Saudi Arabia inamtaka Leandro Trossard. Shida inaweza isiuze.


Chelsea

The Blues ilikuwa kwenye kiwango bora kabisa wakati inaingia Januari, dirisha la usajili ambalo imekuwa ikifanya vizuri kwa miaka ya hivi karibuni. Wakati kukiwa na ripoti Chelsea imelenga kufanya usajili wa straika mwingine wa kuja kumpa ushindani wa namba Nicolas Jackson, ishu nyingine ni kocha Enzo Maresca kutazama na kuendelea kukikuza kiwango cha wachezaji waliopo kwenye timu. Kocha, Maresca atahitaji kupunguza idadi kubwa ya wachezaji huko kwenye mazoezi yake Cobham, walau wachezaji watano wanapaswa kufunguliwa mlango wa kutokea Stamford Bridge, akiwamo Ben Chilwell, ambaye alikuwa analipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na hachezi. Kocha Maresca hahitaji kuongeza mtu, lakini anapaswa kupunguza watu kwenye kikosi chake.


Liverpool

Kocha Arne Slot ameanza maisha yake vyema kabisa kwenye kikosi cha Liverpool kikifanya vyema kwenye Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku ikifika nusu fainali ya Kombe la Ligi. Liverpool imekuwa na msimu mzuri kabisa na pengine kwa sasa inapaswa kubaki na kikosi chake kilichopo na kama kusajili wapya basi wasubiri hadi mwishoni mwa msimu. Kitu pekee wanapaswa kufanya kwenye dirisha hili la Januari ni kumalizana na Federico Chiesa, kwamba inaweza kumfungulia mlango wa kutokea kwenye usajili huu kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuisaidia timu hiyo. Mchezaji mwingine ambaye Liverpool inaweza kumfungulia mlango wa kutokea ni beki wa kati Ibrahima Konate, ambaye amerejea uwanjani siku za hivi karibuni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu alipoumia dhidi ya Real Madrid, Novemba 27 mwaka jana. Mchezaji mwingine ni Joe Gomez, ambaye pia amekuwa akiumia sana.


Man United

Ruben Amorim ana matatizo mengi zaidi kwenye kikosi chake. Kocha huyo Mreno bado hajapata kile anachokitaka kwenye kikosi chake, hivyo anaweza kutumia dirisha hili la uhamisho wa majira ya baridi kutengeneza kikosi chake kwa kuondoa wale ambao anadhani ni mzigo na kuleta wapya ambao wataongeza kitu kipya kwenye timu. Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye hatari ya kuondoka Man United kwenye dirisha hili la Januari ni mshambuliaji Marcus Rashford, ambaye mshahara wake wa Pauni 325,000 anaolipwa kwa wiki, unaweza kuchangia akafunguliwa mlango. Shida ni kupata timu ambayo itakuwa tayari kumsajili Rashford kwa mshahara huo anaolipwa huku pia kikosi hicho kikihusishwa na mpango wa kumsajili straika Victor Osimhen.


Man City

Tangu kiungo Rodri alipoumia na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, kikosi cha Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola kimekuwa kikipata matokeo ya hovyo sana uwanjani. Timu hiyo ilipoteza mechi mfululizo kabla ya kufanikiwa kurudi kwenye hali ya ushindi na kushinda mechi zake mbili za mwisho. Viungo Mateo Kovacic, Ilkay Gundogan na Rico Lewis wote bado hawampi kocha Guardiola kile anachokitaka ndani ya uwanja na ndio maana baada ya dirisha hili la Januari kufunguliwa, miamba hiyo ya Etihad imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi. Mhispaniola huyo aligomea ofa ya Pauni 50 milioni kutoka Liverpool mwaka jana, lakini anaweza kushawishika kwenda kwa Guardiola, Januari hii.


Tottenham

Kocha Ange Postecoglou ameifanya Tottenham Hotspur kuwa timu ya kuburudisha, lakini kwa siku za hivi karibuni timu hiyo imevamiwa na majeruhi wengi ambao wanafanya kikosi hicho kuwa dhaifu na kuchapwa tu. Kutokana na hilo, kikosi hicho kinapaswa kufanya maboresho makubwa kwenye dirisha hili la Januari kwa sababu timu hiyo ina safu nzuri ya ushambuliaji, lakini shida ipo kwenye beki yao, inaruhusu sana mabao. Mabeki Cristian Romero na Micky van de Ven kwa sasa ni majeruhi na Radu Dragusin amekiwa akipata shida kuendana na kasi akicheza na Archie Gray. Kutokana na hilo, kocha Postecoglou anahitaji kufanya usajili wa beki mwingine wa kati kwenye dirisha hili la Januari ili kujenga safu nzuri ya mabeki kuondoa tatizo linalowakabili.