Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars ina dakika 90 za kuandika historia WAFCON

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Baada ya kuishtua Afrika Kusini kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza, Tanzania sasa ina nafasi nzuri ya kusonga hatua ya robo fainali ikiwa itaibuka na ushindi mwingine dhidi ya Burkina Faso.

TIMU ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars ina dakika 90 za kuandika historia mpya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026), itakapovaana na Burkina Faso katika mchezo wa pili wa Kundi B utakaopigwa saa 5 usiku katika Uwanja wa Uwanja wa Larbi Zaouli Stadium.

Mechi nyingine ya kundi B  itazikutanisha Ivory Coast na Afrika Kusini mechi itakayopigwa mapema saa 2 usiku.

Baada ya kuishtua Afrika Kusini kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza, Tanzania sasa ina nafasi nzuri ya kusonga hatua ya robo fainali ikiwa itaibuka na ushindi mwingine dhidi ya Burkina Faso.

Ushindi dhidi ya Burkina Faso utaifanya Twiga Stars kufikisha pointi sita na kuwa na nafasi kubwa ya kufuzu robo fainali moja kwa moja kabla hata ya mchezo wa mwisho dhidi ya Ivory Coast.

Matokeo hayo pia yataongeza presha kwa Afrika Kusini ambayo tayari imeanza mashindano kwa kupoteza na sasa inalazimika kutafuta ushindi dhidi ya Ivory Coast ili kubaki kwenye mbio za kufuzu.

Kwa Twiga Stars, nguvu kubwa imeonekana kwenye nidhamu ya ulinzi, kasi ya kushambulia kwa kushtukiza na matumizi mazuri ya nafasi chache zinazopatikana. Dhidi ya Afrika Kusini, Tanzania ilionyesha utulivu mkubwa licha ya kukabiliwa na presha, jambo lililozaa mabao ya Diana Msewa na Hasnath Ubamba yaliyowapa ushindi muhimu wa kihistoria.

Hata hivyo, Burkina Faso sio timu ya kudharauliwa. Licha ya kufungwa 4-1 na Ivory Coast, timu hiyo ilionyesha uwezo wa kutengeneza nafasi kupitia mashambulizi ya haraka na mipira ya pembeni.

Kabla ya WAFCON, Burkina Faso ilishinda mechi zake zote nne za kufuzu, jambo linaloonyesha kuwa bado ina kikosi chenye uwezo wa kurejea kwenye ushindani.

Udhaifu mkubwa wa Burkina Faso umeonekana kwenye safu ya ulinzi, hasa inapokabiliwa na mashambulizi ya kasi. Mabeki wake walionekana kushindwa kuhimili presha ya washambuliaji wa Ivory Coast na kuacha nafasi nyingi katikati pamoja na pembeni.

Kocha wa Stars, Bakari Shime amesema “Tunafahamu ugumu tutakaokutana nao dhidi ya Burkina Faso imepoteza mechi ya kwanza hivyo inahitaji kufanya vizuri kwenye mechi dhidi yetu hivyo tumejipanga kukabiliana na namna watakavyokuja kwa kuwa na sisi tunahitaji ushindi pia.”