Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakala wa Sesko azipigia simu Liverpool, Man United

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Arsenal ilikuwa tayari kumsajili lakini ilihitaji Leipzig ikubali kushusha ada ya uhamisho ya Euro 90 milioni iliyokuwa ikiihitaji lakini walikataliwa hali iliyosababisa dili kufeli.

WAKALA wa mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 22, amewasiliana na Liverpool ili kujua kama ina nia ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Slovenia, kutokana na uamuzi wa Arsenal kuhamishia nguvu zao kwa mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.

Arsenal ilikuwa tayari kumsajili lakini ilihitaji Leipzig ikubali kushusha ada ya uhamisho ya Euro 90 milioni iliyokuwa ikiihitaji lakini walikataliwa hali iliyosababisa dili kufeli.

Taarifa zinaeleza Liverpool haijatoa jibu lolote hadi sasa na bado mabosi wanatafakari na benchi la ufundi kuona kama wana uhitaji naye.

Mbali ya Liverpool, wawakilishi wa Sesko pia wanazungumza na timu nyingine za Ligi Kuu England ikiwemo  Liverpool, Chelsea, Manchester United na Newcastle United kuonba kama zinaweza kuwa tayari kumsajili fundi huyo.

Sesko mwenyewe anadaiwa alichukizwa na kitendo cha dili lake la kwenda Arsenal kukwama mapema katika dirisha hili, hivyo anataka kuondoka.

Timu nyingi zilivutiwa na kiwango ambacho alikionyesha katika msimu uliopita ambapo alicheza mechi 45 za michuano, akafunga mabao 21 na kutoa asisti sita. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Sesko anatamani sana kupata changamoto mpya sehemu nyingine.


Cristhian Mosquera

BEKI kisiki wa Valencia, Cristhian Mosquera yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na Arsenal dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya kufikia makubaliano binafsi na washika mitutu hao. Mosquera mwenye umri wa miaka 21, anasajiliwa kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuwapa changamoto mabeki wa sasa Gabriel Magalhaes and William Saliba. Arsenal ipo tayari kutoa takriban Euro 25 milioni kama ada yake ya uhamisho na mchezaji mwenyewe ameweka wazi kuwa anaihitaji Arsenal tu.


Pierre Emerick Aubameyang

MABOSI wa Marseille wamefikia hatua nzuri katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Al Qadsiah ya Saudi Arabia, Pierre Emerick Aubameyang katika dirisha hili. Ripoti zinaeleza Kocha wa Marseille, Roberto de Zerbi ndio anahitaji sana huduma ya staa huyu kuelekea msimu ujao. Auba anatarajiwa kuwa atasaini mkataba wa miaka miwili na ataondoka kama mchezaji huru  Al Qadsiah bila ya Marseille kulipa chochote.


John Victor

BOTAFOGO ya Brazil imeingia sokoni kutafuta kipa mpya baada ya Manchester United kuwatumia ofa ya kutaka kumsajili kipa wao raia wa  Brazil, John Victor mwenye umri wa miaka 29. Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, Botafogo ipo tayari kumuuza kipa huyo ingawa mazungumzo bado yanaendelea. Man United imeingia sokoni kusajili kipa mpya baada ya kuumia kwa Andre Onana atakayekuwa nje kwa muda mrefu.


Jesurun Rak-Sakyi

RANGERS inapambana kwa ajili ya kumsajili winga wa Crystal Palace, Jesurun Rak-Sakyi katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Rak-Sakyi mwenye umri wa miaka 22, huduma yake pia inawindwa na timu mbalimbali barani Ulaya ikiwa pamoja na Wolves. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na kuna uwezekana nyota huyo akatimkia Scotland msimu ujao kuanza maisha mapya huko.


Daniel Muno

LICHA ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha Crystal Palace hadi mwaka 2028, beki kisiki wa Palace na timu ya taifa ya Colombia, Daniel Munoz, 29, yupo tayari kuondoka katika kikosi hicho dirisha hili ikiwa ofa nono itawekwa mezani kutoka kwa timu yoyote inayomhitaji. Mkataba wake una kipengele kinachoiwezesha Palace kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa itahitaji kufanya hivyo.


Victor Osimhen

Galatasaray imerudi tena mezani na ofa mpya kwa ajili ya Victor Osimhen, 26 na ipo tayari kutoa Euro 75 milioni lakini itatanguliza kwanza Euro 40 milioni kisha Euro 35 milioni italipa kwa awamu ikianza na Euro 17.5 milioni na kumalizika Euro 17.5 milioni.  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria alicheza Galatasaray kwa mkopo msimu uliopita.


Giorgio Scalvin

ATALANTA inataka ofa ya angalau Pauni 50 milioni kwa timu yoyote itakayohitaji huduma ya beki wao wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 21, Giorgio Scalvini ili kuwauzia dirisha hili. Fundi huyu aliyeonyeha kiwango bora msimu uliopita, huduma yake inahitajika na vigogo mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Newcastle United na Manchester United.