Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachambuzi wanavyoichambua Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Hiyo ilikuwa mechi ya tatu mfululizo ambayo Arsenal imeshuhudia ikiangusha pointi, hali iliyoruhusu Manchester City na Aston Villa kuongeza presha katika mbio za ubingwa baada ya kupunguza pengo la pointi na sasa kubakia nne tu.

LONDON, ENGLAND: MPANGILIO wa timu ya Arsenal chini ya Mikel Arteta umekosolewa vikali baada ya kikosi hicho kupoteza dhidi ya Manchester United kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England kipute kilichopigwa uwanjani Emirates, Jumapili.

Hiyo ilikuwa mechi ya tatu mfululizo ambayo Arsenal imeshuhudia ikiangusha pointi, hali iliyoruhusu Manchester City na Aston Villa kuongeza presha katika mbio za ubingwa baada ya kupunguza pengo la pointi na sasa kubakia nne tu.

Arsenal ilipigwa 3-2 nyumbani uwanjani Emirates mbele ya Man United, wakiruhusu mabao matatu kwa mara ya kwanza tangu ushindi wao wa kusisimua wa 4-3 dhidi ya Luton mnamo Desemba 2023.

Licha ya udhaifu wa ulinzi uliojitokeza, ni safu ya ushambuliaji inayomletea Arteta wasiwasi mkubwa zaidi, huku Gary Lineker, Micah Richards na Alan Shearer wote wakikosoa mbinu zinazotumiwa.

ARS 04

Akizungumza kwenye podikasti ya The Rest Is Football Jumapili jioni, Lineker alianza kwa kusema: “Arsenal, ni kama vile, tusemeje, muda wa kukaza misuli kwa Arsenal. Ni mapema sana kwa hilo, bado wanaongoza vizuri. Yanayumba kidogo kidogo, na ukiangalia nyuma, Man City pia hawako thabiti kwa sasa.

“Aston Villa kwa sasa wanazidi matarajio, wana wachezaji wazuri sana na ni timu imara. Halafu kuna pengo kubwa. Bado nafikiri Arsenal watakuwa sawa.

“Mara kwa mara utapoteza mechi kwa sababu ni vigumu kuepuka hilo.”

Hata hivyo, Richards anaangalia picha kubwa zaidi na hapendezwi na jinsi Arteta anavyowaagiza wachezaji wake kucheza.

Aliyekuwa beki wa Aston Villa na Manchester City amesema: “Naanza kuwa na wasiwasi kidogo kuhusu Arsenal kwa sababu nahisi wanacheza kwa kujilinda sana.

ARS 03

“Sidhani kama hili ni la mechi chache zilizopita tu, limekuwa hivyo kwa sehemu kubwa ya msimu. Wamefunga mabao 13 kutokana na mipira ya adhabu. Mfungaji anayefuata ana mabao matano tu.”

Lineker, akisoma takwimu zilizoonyeshwa awali kwenye Sky Sports wakati wa mechi, aliendelea kuangazia matatizo ya timu hiyo.

Amesema: “Nina jambo bora zaidi hapa Micah, kuhusu washambuliaji na mabao yao. “Bukayo Saka: Hana bao katika mechi 13 za mwisho katika mashindano yote. Viktor Gyökeres: Hana bao lolote lisilotokana na penalti katika mechi 11 za mwisho za Ligi Kuu England.

“Gabriel Martinelli: Hana bao katika mechi 13 za mwisho za Ligi Kuu. Noni Madueke: Hana bao katika mechi 25 za mwisho za Ligi Kuu. Leandro Trossard: Bao moja tu katika mechi 11 za mwisho kwenye mashindano yote.

“Najua wachezaji wengine wamechangia mabao, hasa mabeki, na bila shaka (Eberechi) Eze alifunga hat-trick dhidi ya Tottenham, kwa hiyo hatuwezi kuwasahau waliopata mabao machache. Lakini kwa jumla hawana mchezaji anayefunga mabao kwa uthabiti.”

ARS 02

Mfungaji bora wa Arsenal kwenye ligi ni Gyokeres, lakini mabao matatu tu kati ya hayo amefunga kwa staili isiyokuwa ya mipira iliyokufa.

Kwa jumla, usajili huyo wa Pauni 60 milioni alifunga bao moja tu la ligi dhidi ya timu zilizo nafasi ya 16 au juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.

Hata hat-trick ya Eze inamwacha na bao moja tu la ligi katika mechi nyingine 16, alianza kwenye mechi 10.

Lineker aliendelea kusema: “(Gabriel) Jesus amerudi na amefunga bao moja au mawili, lakini tunajua kuna sababu walihitaji kununua mshambuliaji mwingine Namba 9 mwanzoni. Nampenda Jesus, nimekuwa nikimpenda siku zote, ana bidii kubwa.  Anakimbia, anasumbua mabeki, anafunga mabao kadhaa, lakini si mchezaji wa uthabiti mkubwa. Anapokuwa kwenye kiwango yuko vizuri sana, lakini anaposhuka, anaonekana kuathiriwa kiakili.

“Nilisikia na huenda ni upuuzi mtupu kama mambo mengi mitandaoni, kwamba walihusishwa na Julian Alvarez, ambaye najua hafurahishwi sana na maisha yake Atletico Madrid. Huyo ni aina ya mchezaji anayejua kushughulikia mechi kubwa. Ni mshindi wa Kombe la Dunia. Mchezaji wa aina hiyo, nadhani mchezo ungekuwa umeisha. Lakini wanahitaji mmoja au wawili kati ya washambuliaji hawa waanze kufunga mara kwa mara.”

Barani Ulaya, Arsenal wamekuwa na matatizo machache, huku Martinelli, Gyokeres na Madueke wakifunga kwa uhuru zaidi.

ARS 01

Lakini, Shearer anaamini anajua sababu. Mfungaji bora wa kihistoria wa Ligi Kuu England amesema: “Hawakujilinda sana dhidi ya Inter Milan kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki. Tofauti pekee ni Inter waliwashambulia, ilhali si timu nyingi zinazothubutu kuwashambulia Arsenal.

“Wanapokutana na timu zinazokaa nyuma, wanawategemea zaidi Saka au Trossard kufanya jambo kutokea pembeni, kama ambavyo ilikuwa kwenye mechi ya Man United, nadhani walifanya hivyo, lakini wapinzani wao walikuwa bora zaidi. Kwenye mbinu hiyo, Arsenal huo inapata shida sana.”

Richards aliingilia kati na kupanua hoja hiyo: “Uko sahihi kabisa hapo Alan. Nafikiri hilo linatokana na mabadiliko ya mchezo.

“Arsenal inapojenga mashambulizi, wanajenga kwa mwendo wa taratibu sana, na inapopeleka mpira pembeni, mabeki wanawazunguka kwa wingi.”

Lineker akajibu: “Ni rahisi sana kukabwa unapochelewa kupeleka mpira pembeni. Ukipata mpira huko mapema, una nafasi ya kumkuta Saka akiwa peke yake.”

Richards akajibu tena: “Hilo ndilo jambo lenyewe. Wanakuwa wameanza wakiwa nyuma sana. Ukimwangalia Trossard na Saka, Arsenal inapopoteza mpira wote wanakuwa katika nusu yao na wanapoanza kujenga tena mashambulizi, inachukua muda mrefu sana. Na hili limekuwa likiendelea kwa muda sasa.

“Ni rahisi kuangalia idadi ya washambuliaji na kusema ndiyo, Gyokeres angefanya vizuri zaidi. Saka tunajua siku zote anacheza vizuri na kujaribu kuunda kitu, lakini analazimika kufanya hivyo akiwa nyuma sana. Inakuwa kazi ngumu sana kwake.”

Lineker, ambaye mwenyewe alijua vyema kufunga mabao, alimpongeza Saka lakini alikiri matatizo bado yapo.

Amesema: “Kila wakati anakabiliwa na wachezaji wawili, na kwa kushangaza bado anaweza kuwapita, lakini anapofanikiwa, tayari kila mtu amejipanga na hakuna nafasi.”

Richards alihitimisha: “Hili limekuwa likitokea kwa muda sasa, na wamekuwa wakipata bao la mpira wa adhabu ndipo mchezo unafunguka na timu pinzani inalazimika kushambulia. Lakini kwa sasa inakatisha tamaa kuwaona wachezaji wako wabunifu wakilazimika kufanya kazi nyingi sana za ulinzi huku wakisubiri mipira ya adhabu kuweza kuwafungua wapinzani kwenye nafasi zao wanazokaba.”