Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Dewji aahidi mambo mawili Simba

MAWILI Pict


MWEKEZAJI wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ amesema bado ana madeni mawili kwenye timu hiyo.


MO ambaye alianza kuwekeza Simba tangu mwaka 2017, ni mmoja kati ya watu walioisaidia timu hiyo kuwa na mafanikio makubwa nje na ndani ya uwanja kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.


Mwekezaji huyo ambaye ni mbunge wa zamani wa Singida Mjini, amesema Simba ni timu kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, lakini kwenye kipindi chake cha miaka 80 ya mwanzo haikuweza kufanya mambo makubwa sana.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu kuelekea maadhimisho ya miaka 90 ya Simba, MO amesema kuna mambo mawili ambayo bado hajayatimiza kwenye timu hiyo na ni lazima apambane nayo kwenye kipindi cha miaka kumi ijayo ili kila kitu kiwe vizuri.

“Simba ni timu kubwa, ina heshima kubwa na kila mmoja amekuwa akiizungumzia kwa sasa kutokana na mafanikio yake, lakini kwa kipindi changu cha uwekezaji kuna mambo mawili bado sijayafanya,” amesema MO ambaye mbali na uwekezaji wake amekuwa akitoa fungu kwenye kila dirisha la usajili kwa ajili ya kusajili mastaa kwenye timu hiyo.

“Jambo la kwanza ni uwekezaji wa miundombinu, natakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa hili eneo linafanyiwa kazi vizuri kwenye kipindi cha miaka 10 ijayo.’’

Mwekezaji huyo amesema kuwa mbali na suala la uwekezaji, jambo lingine ambalo ni deni kwake na anatakiwa kulitimiza kwa miaka kumi ijayo hadi Simba itakapoadhimisha miaka 100 ni kuhakikisha kuwa timu hiyo inatwaa ubingwa wa Afrika.

“Simba ni timu kubwa, ina historia kubwa na mashabiki wazuri sana, lakini kwenye miaka 80 iliyopita haikufanya mambo makubwa ilikuwa imepiga hatua ndogo sana Afrika.

“Kwenye hii miaka 10 ya mwisho hadi kufikia 90 ndiyo Simba imejulikana ulimwenguni kutokana na kufanya vizuri kwenye mashindano ya nje lakini kujitangaza.

“Ukweli ni kwamba bado hatujaridhika na shabaha yangu imebaki palepale, naahidi kuwa Mungu akinipa afya njema, kwa miaka kumi ijayo, Simba Inshallah tutatwaa ubingwa wa Afrika.’’ amesema MO. Hata hivyo, MO amesema hayo yatatokea endapo kila mmoja atakuwa na afya njema, anatamani ‘Transformation’ ikikamilika, uwekezaji ukifanyika basi kila kitu alichoahidi kitafanyika bila shida yoyote.

Mo amesema kabla ya kufanya uwekezaji mwaka 2017, klabu hiyo kwenye ramani ya soka barani Afrika haikuwepo hata kwenye timu 100 bora.

“Ukiona hii leo tumekuwa kati ya timu tano mpaka 10 bora Afrika, ujue kuna kazi kubwa imefanyika kwenye hii miaka minane, tisa kumi iliyopita lakini shabaha ni kupata taji la Afrika ingawa ni lazima tufanya kazi kubwa sana kama tunataka mafanikio hayo,’’ amesema MO ambaye anakiri kuwa yeye ni shabiki wa Simba tu.

Pia rais huyo wa heshima ametoa wito kwa wanachama na mashabiki wa Simba kuachana na maneno ya chuki na badala yake wajikite katika mshikamano, kushirikiana na kujenga klabu kwa pamoja.

MO ambaye leo atakuwa akiifuatilia Simba ikiadhimisha kileleni cha Simba Day kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, amekuwa akikiri mara kwa mara kuwa anawekeza kwenye klabu hiyo kwa ajili ya mapenzi na siyo jambo lingine.

“Nimewekeza muda, jasho, damu na fedha Simba. Sio kwa sababu nyingine, bali kwa mapenzi ya dhati kwa klabu hii na kwa taifa letu. Ndoto yangu haijabadilika.”