Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya namba Jesus, Gyokeres Arsenal

Muktasari:

  • Hata hivyo, takwimu kutoka San Siro zinaonyesha wazi kuwa Jesus angekuwa chaguo bora kwa Arsenal kuelekea mchezo wao muhimu dhidi ya Manchester United kwenye Ligi Kuu England, Jumapili.

LONDON, ENGLAND: MASTRAIKA, Gabriel Jesus na Viktor Gyokeres wote waliandikisha majina yao kwenye orodha ya wafungaji katika ushindi wa Arsenal wa mabao 3-1 dhidi ya Inter Milan Jumanne usiku katika mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, takwimu kutoka San Siro zinaonyesha wazi kuwa Jesus angekuwa chaguo bora kwa Arsenal kuelekea mchezo wao muhimu dhidi ya Manchester United kwenye Ligi Kuu England, Jumapili.

Arsenal ya kocha Mikel Arteta iliandikisha ushindi wao wa saba katika mechi saba za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwapiga mabao 3-1 mabingwa wa Serie A shukrani kwa mabao mawili mazuri ya Jesus katika kipindi cha kwanza. Shoo hiyo ya Jesus inamweka Gyokeres kwenye presha mkubwa, ambaye alianza mchezo huo akiwa benchini, hasa baada ya kufunga bao moja tu katika mechi zake 10 za mwisho.

Hata hivyo, Gyokeres, aliyesajiliwa kwa Pauni 63.5 milioni aliwanyamazisha wakosoaji kwa kufunga bao zuri la mkwaju wa kupinda kuelekea juu ya kona ya lango, na kuupamba zaidi ushindi huo wa Arsenal na sasa kuibua mjadala nani aanze kati yao katika mechi ya Man United, Emirates Jumapili.

Gyokeres ameanza mechi nane za mwisho za Arsenal kwenye Ligi Kuu England, lakini kurejea kwa Jesus kwenye kiwango bora kunamaanisha ushindani mkali sasa umeibuka katika nafasi ya mshambuliaji. Na bila shaka, kiwango cha Jesus dhidi ya Inter kitaongeza nafasi zake kuanza dhidi ya Man United.

Jesus alicheza dakika 75, akifunga mashuti yake yote mawili, akishinda mapambano manne na kugusa mpira mara 28 kwa jumla.

Mchambuzi mmoja alisema: “Hatimaye huu ni uamuzi mkubwa kwa Mikel Arteta. Je ataendelea na Gabriel Jesus kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Man United, au atamrudisha Viktor Gyokeres kwenye kikosi baada ya bao lake la kujenga kujiamini, la tisa tangu ajiunge kutoka Sporting Lisbon?

Ni uamuzi mkubwa sana, lakini mimi najua ningefanya nini, ningemchagua Gabriel Jesus kwa sababu Arsenal huonekana bora zaidi akiwa ndani.”

Jesus pia alichangia kwa ubunifu kwa kutengeneza nafasi mbili za kufunga na kupiga pasi 10 zilizofanikiwa kuelekea nusu ya uwanja wa wapinzani. Kwa kulinganisha, Gyokeres naye alipiga mashuti mawili, akashinda pambano moja tu na kugusa mpira mara nane. Lakini, Gyokeres alipata muda mchache zaidi uwanjani, akicheza dakika 15 za mwisho.

Hata hivyo, ramani zao za maeneo waliyochezea zinaonyesha tofauti kubwa, ambapo Jesus alionekana akicheza pembeni, akirudi chini kusaidia timu na kufunika maeneo mengi ya uwanja, wakati upande wa Gyokeres, ramani yake ilionyesha kuwa mara nyingi alibaki katikati ya uwanja.