Vigogo Real Madrid waweka mzigo kwa Rodri
Muktasari:
- Awali, iliripotiwa kuwa inamhitaji lakini tetesi zikafifia hususani baada ya staa huyu kupata majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
REAL Madrid iko tayari kutoa Pauni 100 milioni kwenda Manchester City kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya Hispania, Rodri katika dirisha hili la majira ya kiangazi.
Awali, iliripotiwa kuwa inamhitaji lakini tetesi zikafifia hususani baada ya staa huyu kupata majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Madrid imerejea na ofa hiyo, pia inataka kumpa mshahara mnono ambao utamfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaokunja pesa nyingi katika kikosi chao.
Vilevile, kocha mpya wa Madrid, Xabi Alonso, amemtaja kiungo huyo Mhispania kuwa kipaumbele chake cha kwanza katika eneo la kiungo.
Ingawa Man City haitaki kumuuza kiungo huyu ambaye amekuwa ni mhimili katika aneo la katikati ya kiwanja, Madrid inaamini huenda wakashawishika ikiwa itaweka dau kubwa.
Taarifa kutoka The Sun zimefichua kwamba Alonso anashinikiza uongozi wa Madrid kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya fundi huyo mwenye umri wa miaka 29.
Mkataba wa Rodri na Man City unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na katika michuano ya Kombe la Dunia kwa Klabu iliyofanyika huko Marekani, Rodri alicheza mechi nne za michuano yote na kutoa asisti moja.
Jack Grealish
WINGA wa Manchester City na England, Jack Grealish mwenye umri wa miaka miaka 29, bado yupo katika rada za Napoli inayohitaji kumsajili katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ushambu-liaji.
Grealish ni miongoni mwa wachezaji waliopewa barua za kutafuta timu na Man City kwani hayupo kati-ka mipango ya kocha Pep Guardiola kwa ajili ya msimu ujao.
Javi Guerra
KIUNGO wa Valencia, Javi Guerra amekataa ofa ya kuongezewa mkataba na timu hiyo katika dirisha hili ikidaiwa anataka kuondoka na kutua Manchester United ambayo imeshaanza mazungumzo na wa-wakilishi wake.
Guerra mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 38 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti tatu.
Kobbie Mainoo
TOTTENHAM inamfuatilia kwa karibu kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo, katika dirisha hili baada klabu yake kuweka wazi kwamba ipo tayari kumuuza.
Mainoo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027, anaripotiwa kugoma kusaini mkataba mpya na kwa sababu hiyo, Man United inataka kumuuza sasa ili kuepuka hasara ya kumuuza kwa pesa pun-gufu mwakani.
Douglas Luiz
WEST Ham imeingia katika vita dhidi ya Everton ili kuipata saini ya kiungo wa Juventus, Douglas Luiz iki-wa ni siku kadhaa tu tangu Aston Villa kujiondoa kwenye mbio za kutaka kuipata saini yake katika diri-sha hili.
Staa huyu wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, mara kadhaa pia amekuwa akihusishwa na Manchester United. Mkataba wake na Juventus unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.
Federico Chiesa
ATALANTA inapanga kufanya jaribio la kumsajili winga wa Liverpool na Italia, Federico Chiesa mwenye umri wa miaka miaka 27, ikiwa itapata pesa ya kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Ade-mola Lookman kwenda Juventus katika dirisha hili. Mabosi wa Atalanta wana matumaini ya kumuuza Chiesa kwa Euro 50 milioni na pesa hiyo ndio itaitumia kufanya usajili wa wachezaji wengine wanaowa-hitaji.
Callum Wilson
INAELEZWA West Ham ipo katika mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji aliyemaliza mkataba Newcastle United, Callum Wilson ili kumsajili staa huyo katika dirisha hili kwa uhamisho wa bure.
Callum mwenye umri wa miaka 33, msimu uliopita alicheza mechi 22 za michuano yote na amepoteza namba kikosini.
Joao Palhinha
TOTTENHAM inajiandaa kuwasilisha ofa kwenda Bayern Munich kwa ajili ya kuipata huduma ya kiungo wa klabu hiyo, Joao Palhinha ili kumsajili katika dirisha hili.
Palhinha mwenye umri wa miaka 30, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Mabosi wa Bayern wapo tayari kumruhusu staa huyu aondoke.