Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo kibao Serie A wamtaka Harry Maguire

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Maguire amekuwa akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Man United jambo linalodaiwa kumfanya afikirie kuondoka kwa sababu anahofia nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kupigwa baadaye mwaka huu huko Marekani, Canada na Mexico.

INTER Milan, Napoli na Fiorentina zimeingia vitani kuwania saini ya beki wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Harry Maguire, 32, katika dirisha hili la usajili.

Maguire amekuwa akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Man United jambo linalodaiwa kumfanya afikirie kuondoka kwa sababu anahofia nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kupigwa baadaye mwaka huu huko Marekani, Canada na Mexico.

Timu hizo zinamuona Maguire kuwa beki mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza timu kama mchezaji mzoefu.

Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu na tangu kuanza kwa msimu huu akiwa Old Trafford amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

Taarifa zinadai Napoli imekuwa ikijaribu kuwatumia wachezaji wa zamani wa Man United Scott Mctominay na Rasmus Hojlund ili ya kumshawishi akubali kujiunga nao.


Jean-Philippe Mateta

JUVENTUS imeanza mawasiliano ya awali na Crystal Palace kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28, ambaye inamuona kuwa mrithi wa muda mrefu wa straika  wa kimataifa wa Serbia, Dusan Vlahovic, 25, ambaye tangu mwaka jana amekuwa akihusishwa kuondoka.

Mateta ambaye pia aliwahi kuhusishwa na Man United mara kadhaa mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027 na Palace haina haraka ya kumuuza.


Tammy Abraham

ASTON VILLA inataka kuhakikisha inamsajili moja kwa moja mshambuliaji raia wa England, Tammy Abraham, 28, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Besiktas akitokea Roma.

Abraham alicheza Villa 2018/19 alikosajiliwa kwa mkopo akitokea Chelsea kuisaidia timu hiyo kupanda daraja kwenda Ligi Kuu England, akifunga mabao mawili katika mechi ya mwisho iliyoiwezesha kuvuna pointi za kupanda. Mabosi wa Villa wanamkubali na wana imani ataungana nao.


Murillo

MANCHESTER United imeanza kumfuatilia kwa karibu beki wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Brazil, Murillo, 23. Murillo amevutia timu nyingi ambazo zimekuwa zikimiminika kutaka kumsajili tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini changamoto inaonekana kuwa kwa Forest ambayo haitaki kumuuza kwa sasa. Vigogo wa Old Trafford wanaamini Murillo wakimnasa ni uwekezaji wa muda mrefu.


Bernardo Silva

KIUNGO mshambuliaji wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva, 32, ameendelea kuwa gumzo katika soko la usajili la Januari ambapo Galatasaray, Napoli, Juventus pamoja na timu kadhaa za Saudi Arabia zimeendelea kumfuatilia kwa karibu na kuulizia ikiwa zinaweza kumpata.

Silva yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na bado hajaafikiana na Man City kuhusu kuongeza mkataba mpya.


Frank Onyeka

MIAMBA ya soka ya Hispania, Valencia imeripotiwa kubisha hodi  Brentford kuulizia uwezekano wa kunasa saini ya kiungo Mnigeria Frank Onyeka.

Valencia inahitaji huduma ya staa huyo,28, baada ya kuonyesha kiwango bora katika Afcon 2025, ambako Super Eagles ilikomea kwenye hatua ya nusu fainali.

Hivi karibuni, Onyeka alifichua kuwa ndoto zake ni kujiunga Manchester United ambayo imekuwa moyoni mwake.


Sidiki Cherif

CRYSTAL PALACE ipo katika mazungumzo na Angers ya Ligue 1 juu ya uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Ufaransa, Sidiki Cherif, 19.

Cherif ni mchezaji anayeweza kucheza katikati kama mshambuliaji namba tisa na pia pembeni kama winga, na tangu kuanza ka msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao manne. Mkataba anamalizika 2028.


Ross Barkley

SHEFFIELD UNITED imeanza harakati za kumsajili kiungo wa kimataifa wa England, Ross Barkley, 32, ambaye kwa sasa anakosa muda wa kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha Aston Villa.

Barkley, aliyeichezea Everton, Chelsea na Luton Town anaamini ana uwezo mkubwa wa kucheza Ligi Kuu England, lakini kuendelea kuwa benchi kunadaiwa kumfikirisha kufanya uamuzi wa kujiunga na Sheffield.