Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo England vikumbo tu, vita bado mbichi kwa Guehi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na taarifa zinadai mabosi wa Palace wanataka kumuuza baada ya kuona hataki kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo.

ARSENAL ipo tayari kuingia katika vita dhidi ya Manchester City na timu nyingine za Ligi Kuu England ili kuipata saini ya beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi katika dirisha hili la majira ya baridi.

Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na taarifa zinadai mabosi wa Palace wanataka kumuuza baada ya kuona hataki kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo.

Guehi ni miongoni mwa mabeki waliokuwa karibu kujiunga na Liverpool katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini dili lilifeli katika dakika za mwisho baada ya kocha kuzuia.

Mabosi wa Man City wameingia katika mpango wa kutaka kumsajili Guehi dirisha hili baada ya mastaa wengi kupata majeraha yanayotarajiwa kuwaweka nje kwa muda mrefu.

Guehi, 25, hajaonyesha ishara kulazimisha kuondoka.




Danilho Doekhi

BEKI wa kati wa Union Berlin na timu ya taifa ya Uholanzi, Danilho Doekhi, mwenye umri wa miaka 27, anaripotiwa kutaka kujiunga na Leeds United ambayo imewasilisha ofa ya kutaka kumsajili.

Doekhi anataka kufanya kazi chini ya kocha Daniel Farke ambaye amemhakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Bado Leeds United inaendelea kufanya mazungumzo ili kumsajili.


Antonio Rudiger

REAL Madrid ipo tayari kumuuza beki wa kati wa kimataifa wa Ujerumani, Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 32, kwa ada ya Euro 10 milioni katika dirisha hili la Januari.

Mkataba wa Rudiger unatarajiwa kumalizika katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, jambo linalowalazimu mabosi wa Real Madrid kutaka kumuuza ili asiondoke bure. Chelsea na Paris St-Germain zinamtaka.


Michael Kayode

MANCHESTER City imeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kulia wa Brentford na timu ya taifa ya vijana ya Italia, Michael Kayode, mwenye umri wa miaka 21.

Mchezaji huyo amelivutia benchi la ufundi la Manchester City kutokana na kasi, nguvu na uwezo alivyoonyesha katika msimu huu wa mashindano huko England.

Manchester City pia inamuona Kayode kama sehemu ya mipango ya muda mrefu kutokana na umri wake kuwa mdogo.


Omar Marmoush

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Misri, Omar Marmoush, mwenye umri wa miaka 26, hana mpango wa kuondoka Manchester City katika dirisha hili la usajili la Januari.

Marmoush anadaiwa kuwa amedhamiria kubaki Etihad na kupambania namba katika kikosi cha kwanza cha wababe hao licha ya ushindani mkubwa uliopo. Nyota huyo anaamini bado anaweza kuwa na nafasi ya kudumu.


Nico Schlotterbeck

REAL Madrid imeongeza kasi katika harakati za mchakato wa kumsajili beki wa kati wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26.

Real Madrid imefanya hivyo baada ya kuona Bayern Munich haitaki kumuuza beki wa kimataifa wa  Ufaransa, Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia yupo karibu kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia.


Mateus Mane

WOLVES imeweka msimamo mkali wa kutomuuza kiungo kinda wa timu ya taifa ya vijana ya England, Mateus Mane, mwenye umri wa miaka 18, katika dirisha hili la Januari.

Klabu hiyo imesisitiza kuwa mchezaji huyo hayupo sokoni kwa bei yoyote kutokana na imani kubwa waliyo nayo juu ya kipaji chake.

Mane anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji wanaoweza kufanya makubwa hapo baadaye.


Souza

TOTTENHAM Hotspur imefikia makubaliano binafsi na beki wa kushoto wa Santos na timu ya taifa ya vijana ya Brazil, Joao Victor de Souza Meneze maarudu Souza mwenye umri wa miaka 19 ambaye anaweza kujiunga na kikosi hicho katika dirisha hili.

Inadaiwa makubaliano ya mchezaji na Spurs tayari yameshafikiwa na sasa Spurs inasubiri hatua zinazofuata kuhusu makubaliano kati ya klabu yao na Santos ambayo inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 30 milioni ili kumuuza.