Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tyson Fury amchapa mtu

FURRY Pict

Muktasari:

  • Wach alishindwa kuendelea na pambano baada ya kumalizika kwa raundi ya saba, huku akiamua kubaki kwenye kona yake, jambo lililompa Fury ushindi wa kishindo katika pambano la raundi 10.

LOS ANGELES, MAREKANI: BONDIA  nyota wa uzani wa juu kutoka England, Tyson Fury, ameonyesha ubabe wake baada ya kumchapa Mpolandi Mariusz Wach kwa TKO katika raundi ya saba kwenye pambano lililofanyika jana Ijumaa usiku nchini Thailand.


Wach alishindwa kuendelea na pambano baada ya kumalizika kwa raundi ya saba, huku akiamua kubaki kwenye kona yake, jambo lililompa Fury ushindi wa kishindo katika pambano la raundi 10.


Fury alitawala pambano hilo tangu mwanzo hadi mwisho dhidi ya Wach, ambaye yuko nje ya orodha ya mabondia 200 bora duniani. Katika raundi ya tano, Fury alionekana kumshambulia mpinzani wake kwa mfululizo wa ngumi tano za uppercut, zilizomweka kwenye wakati mgumu.

FUR 01

Ingawa pambano hilo halikurushwa na vituo vikubwa vya televisheni na halikuvutia mashabiki wengi kama ilivyo kwa mapambano makubwa ya Fury, lilitimiza lengo la kumuweka bondia huyo kwenye ubora wa ushindani kuelekea pambano kubwa linalotarajiwa dhidi ya Anthony Joshua baadaye mwaka huu.


Mbali na mapambano, tukio hilo lilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi ya Father Ray Foundation, ambapo mapato yote ya tiketi kutoka kwa mashabiki wapatao 1,500 yalitolewa kusaidia watoto yatima, wenye ulemavu na vijana wasiojiweza nchini Thailand.

FUR 02

Baada ya ushindi huo, macho sasa yanaelekezwa Saudi Arabia ambako kuna taarifa kuwa waandaaji wa mapambano kutoka kampuni ya Sela wameandaa safari ya Fury kuelekea Jeddah kushuhudia pambano la Anthony Joshua dhidi ya Kristian Prenga lililofanyika leo Jumamosi.


Joshua anarejea ulingoni kwa mara ya kwanza tangu apate ajali mbaya ya gari iliyosababisha vifo vya marafiki zake wawili waliokuwa sehemu ya timu yake ya karibu.


Bondia huyo amesema kipindi hicho kilikuwa kigumu zaidi maishani mwake na ameahidi kuendeleza ndoto walizokuwa nazo pamoja, huku pia akiendelea kuzisaidia kifedha familia zao.

FUR 03

Hata hivyo, bado haijafahamika kama Fury atahudhuria pambano hilo na kukutana ana kwa ana na Joshua, licha ya tetesi zinazoendelea kwamba wawili hao wanaweza kushiriki jukwaa moja kwa mara ya kwanza kabla ya pambano lao linalosubiriwa kwa hamu.


Awali Fury alinukuliwa akisema hana mpango wa kusafiri kwenda Saudi Arabia. Inaaminika anafuata mkakati alioutumia Joshua mapema mwaka huu, ambapo Joshua hakupanda ulingoni baada ya ushindi wa Fury dhidi ya Arslanbek Makhmudov kwa sababu makubaliano ya pambano lao hayakuwa yamekamilika rasmi.


Sasa, ikiwa Joshua atafanikiwa kumshinda Prenga bila matatizo, kuna matumaini makubwa kwamba wawili hao hatimaye watakutana hadharani, hatua ambayo itakuwa ishara muhimu kuelekea pambano kubwa zaidi la uzani wa juu linalosubiriwa na mashabiki wa ngumi duniani.