Bondia Wilder, Tyson Fury wathibitisha kurudiana Julai
Muktasari:
Wawili hao walitoka sare katika pambano lao la kwanza 2018, kabla ya Fury kumchapa Wilder katika raundi ya saba na kushinda taji la WBC kwenye ukumbi wa Las Vegas mwezi uliopita.
London, England. Bondia Deontay Wilder na Tyson Fury watarudiana kwa mara ya tatu baada kambi ya Wilder kuthibitisha kuomba mechi ya marudiano.
Promota wa Fury, Bob Arum amethibisha kwamba mabondia hao watarudiani katikati ya Julai.
Arum aliiambia Ringside: 'Wilder na wawakilishi wake watutumia ujumbe jana usiku wapo tayari kwa ajili ya mechi ya marudiano.
“Pambano hilo litafanyika katikati ya mwaka huu kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki. Itakuwa katikati ya Julai.'
Wawili hao walitoka sare katika pambano lao la kwanza 2018, kabla ya Fury kumchapa Wilder katika raundi ya saba na kushinda taji la WBC kwenye ukumbi wa Las Vegas mwezi uliopita.
Wilder alikuwa na siku 30, za kuomba kurudiana ndicho ilichofanya kambi yake katika kuhakikisha bondia wao anacheza kwa mara ya tatu na Fury.
Wilder mwenye miaka 34, alikuja na kisingizio kuwa kipigo alichokipata kutoka kwa Fury, kimetokana na kuvaa mavazi yenye uzito mkubwa yaliyosababisha miguu yake kukosa nguvu.
Uamuzi huo umefanya kuchelewa kwa pambano baina ya Fury na Anthony Joshua lililokuwa likisubiliwa kwa hamu.
Joshua sasa atazichapa na bondia Mbilgaria Kubrat Pulev katika kutetea ubingwa wa IBF pambano litakalofanyika London hapo Juni 20.