Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trent Alexander-Arnold anaweza kurudi Livepool

TRENT Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anaonekana kuwa chaguo bora ya beki wa kulia, hasa kutokana na kushindwa kwake kuonyesha kiwango bora msimu wake wa kwanza Real Madrid, huku klabu hiyo ikiwa imemsajili Mholanzi Denzel Dumfries kwa ajili ya nafasi hiyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL inapambana kuimarisha kikosi katika dirisha hili la usajili, na ripoti kutoka England zinaonyesha kwamba klabu hiyo “inamhitaji” Trent Alexander-Arnold aliyetimkia Real Madrid msimu uliopita.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anaonekana kuwa chaguo bora ya beki wa kulia, hasa kutokana na kushindwa kwake kuonyesha kiwango bora msimu wake wa kwanza Real Madrid, huku klabu hiyo ikiwa imemsajili Mholanzi Denzel Dumfries kwa ajili ya nafasi hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu England, Gabby Agbonlahor, ameeleza kuna uwezekano wa Alexander-Arnold kurejea Liverpool na kutoa sababu alipozungumza na Ade Oladipo katika kipindi cha Drive.

“Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba ukiitazama Liverpool sasa inamhitaji. Wanamhitaji Trent kuliko hapo awali. Tayari wana namba yao tisa, mshambuliaji wao bora, na Salah hayupo tena. Isak ndiye mchezaji muhimu. Anahitaji nini? Mipira mizuri ya krosi. Hataipata kutoka kwa Frimpong,” amesema.

Agbonlahor pia alimkosoa Frimpong akisema ni beki wa pembeni mwenye kasi na uwezo wa kuwapita wapinzani, lakini ana upungufu katika ulinzi. “Hajui kulinda. Nimemuona akicheza mmoja dhidi ya mmoja katika ulinzi, na hajui kujihami. Mipira yake ya mwisho ni mibaya. Hivyo hata Isak anaweza kuwa anafikiria kwamba wanahitaji kuboresha krosi kutoka upande huo wa kulia,” amesema.

Siyo mara ya kwanza kwa jina la Trent kutajwa anaweza kurejea Liverpool na mchezaji wa zamani, Andy Townsend alikaririwa msimu uliopita akidai: “(Trent) hahitaji msimu mwingine kama ule aliokuwa nao mara ya mwisho. Huenda ilimuumiza kidogo kuona mambo hayakwenda kama alivyotarajia, hayakuanza vizuri na pia akakumbwa na matatizo ya majeraha.”

Townsend anaamini Liverpool inapaswa kujaribu kumrejesha kwa mkopo.

Amesema: “Nadhani Liverpool inapaswa, kama inaweza kufikia makubaliano ya kumchukua kwa mkopo wa msimu mmoja hata kama ada ya sasa inaweza kufikia Pauni 10 milioni kwa msimu, isikose fursa hiyo ya kumrudisha. Ni mchezaji wa kiwango cha juu sana.”