Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu 12 Ulaya zapiga hodi Man United kumtaka Kobbie Mainoo

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mainoo ambaye mkataba wake unamalizika 2027, anataka kuondoka Old Trafford kwa sababu hapati nafasi ya kucheza na kocha Ruben Amorim haonekani kumwamini. Hata hivyo, licha ya kutochezeshwa mara kwa mara mabosi wa Man United wamekuwa wagumu kumruhusu kuondoka.

KIUNGO wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, 20, anawindwa na timu 12 Ulaya ambazo zinasubiri kwa hamu kuona kama mabosi wa Man United watakuwa tayari kumwachia staa huyo katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Awali, Napoli ndio ilionekana kutajwa sana, lakini sasa kuna msululu wa timu ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili.

Mainoo ambaye mkataba wake unamalizika 2027, anataka kuondoka Old Trafford kwa sababu hapati nafasi ya kucheza na kocha Ruben Amorim haonekani kumwamini. Hata hivyo, licha ya kutochezeshwa mara kwa mara mabosi wa Man United wamekuwa wagumu kumruhusu kuondoka.

Kiungo huyo aliomba kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini ombi lake lilikataliwa.

Mainoo anaamini ana nafasi ya kucheza katika Kombe la Dunia lijalo katika kikosi cha England na ili kuhakikisha hilo linafanikiwa itabidi aondoke Januari na kujiunga na timu ambayo itamchezesha mara kwa mara.


Axel Disasi

OLYMPIQUE Lyon inafanya mazungumzo na wawakilishi wa Chelsea na wakala wa beki wa Axel Disasi, ikiwa ni katika mpango wa kutaka kumsajili staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27.

Mabosi wa Lyon wamepata matumaini ya kumsajili Disasi kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Chelsea, hivyo hata yeye mwenyewe anaonekana kutamani kuondoka.


Elliot Anderson

NOTTINGHAM Forest inafikiria kuongeza bei ya kiungo Elliot Anderson kufikia Pauni 100 milioni. Anderson ambaye huduma yake inahitajika na Manchester United na Man City ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Forest na mabosi wa timu hiyo hawataki kuona akiondoka kwa bei ya kawaida kwani itakuwa ngumu kutafuta mbadala wake. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.


Nilson Angulo

MANCHESTER United na Tottenham Hotspur ni miongoni mwa timu za England ambazo zinahitaji saini ya mshambuliaji wa Anderlecht,  Nilson Angulo, 22, katika dirisha lijalo.

Staa huyo wa kimataifa wa Ecuador ameonyesha kiwango bora tangu msimu uliopita. Mkataba wake unamalizika 2029 na msimu huu amecheza mechi 22 akifunga mabao manne na asisti nane.


Ayyoub Bouaddi

KIUNGO wa Lille, Ayyoub Bouaddi yupo katika rada za timu kubwa Ulaya ikiwemo Arsenal ambayo inaonekana kumtolea macho zaidi.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 18, amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Lille tangu apandishwe kutoka kwa vijana na kiwango chake ndicho kinachochanganya vigogo.

Maskauti wa timu mbalimbali wamekuwa wakihudhuria baadhi ya mechi za Lille kwa ajili ya kumtazama.


Yuri Alberto

EVERTON na West Ham United zimeulizia uwezekano wa kumsajili straika wa Corinthians, Yuri Alberto katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu. Alberto, 24, ni miongoni mwa washambuliaji wanaoongoza kwa mabao katika Ligi Kuu Brazil akiwa nayo 18 katika mechi 54 za michuano yote.

Ili kumuuza Corinthians inaweza kuhitaji hadi Pauni 30 milioni.


Tino Livramento

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa Newcastle United, Tino Livramento, 23, anaendelea kuwindwa na Manchester City ambayo inaonekana kuongoza licha ya uwepo wa Manchester United na Arsenal ambazo pia zinamtaka. Livramento ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza Newcastle na timu nyingi zimevutiwa na uwezo wa kutengeneza mashambulizi.


Kenan Yildiz

ARSENAL imeripotiwa kufikia hatua nzuri katika mazungumzo binafsi na  wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uturuki, Kenan Yildiz, 20, anayeichezea Juventus.

Inaelezwa Arsenal inataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Yildiz ambaye ameonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Juventus, amekuwa akihusishwa na timu nyingi tangu dirisha lililopita.