Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Crystal Palace kusikilizia ofa za Mateta

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mateta ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 amekuwa akiwindwa na vigogo wengi tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

CRYSTAL Palace imepanga kusikiliza ofa kutoka timu zinazohitaji huduma ya mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28, kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi.

Mateta ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 amekuwa akiwindwa na vigogo wengi tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyu matata, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 23 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti mbili.

Mapema mwaka huu alikuwa akitajwa kwamba huenda angejiunga na Manchester United iliyokuwa ikitafuta mshambuliaji, lakini baadaye dili likafeli na mashetani wekundu hao wakahamia kwa mastaa wengine.

Kwa sasa AC Milan ndio inaonekana kumtamani zaidi na imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake.

Mateta ameripotiwa kuomba kuachiwa kwa ajili ya kupata changamoto mpya sehemu nyingine, akivutiwa zaidi na aina ya ofa ambazo timu zinazomhitaji ziliweka mezani.

Mabosi wa Palace hawaonekani kuwa na nia ya kumzuia kuondoka ingawa kwa sasa inaweza ikahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni kutokana na kiwango ambacho amekionyesha tangu kuanza kwa msimu huu.


Samuel Chukwueze

FULHAM italazimika kulipa Euro 28 milioni kwenda AC Milan ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja kiungo wa timu hiyo na Nigeria, Samuel Chukwueze, mwenye umri wa miaka 26, ambaye anacheza katika kikosi chao kwa mkopo.

Chukwueze, ambaye alijiunga na Fulham kwa mkopo msimu huu, amekuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hiyo. Mkataba wake na Milan unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Nathaniel Brown

MANCHESTER United, Arsenal na Real Madrid zinapigana vikumbo ili kuipata saini ya beki wa Eintracht Frankfurt, Mjerumani Nathaniel Brown, mwenye umri wa miaka 22.

Brown ambaye anacheza kama  beki wa kati ana nguvu na urefu ambao unamwezesha kuwa imara sana inapokuja mipira juu. Mabosi wa Frankfurt wanaripotiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 40 milioni ili kumuuza mchezaji huyo ambaye msimu huu amecheza mechi 18.


Igor Thiago

TOTTENHAM, Newcastle na Aston Villa zimeanza mchakato wa kuwasilisha ofa ili kumnunua mshambuliaji wa Brentford, Igor Thiago, mwenye umri wa miaka 24 katika dirisha la Januari mwakani.

Thiago, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, katika dirisha lililopita pia alitajwa kwamba anaweza kutua Newcastle na Spurs lakini dili hilo halikufanikiwa.


Sacha Boey

BAYERN Munich ipo tayari kufanya mazungumzo ya kumuuza beki wao wa kulia kutoka Ufaransa, Sacha Boey, 25, kwa ada ya Euro 15 milioni katika dirisha lijalo la majira ya baridi ambapo Crystal Palace tayari imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Boey amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Bayern, akikosa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha wababe hao.

Monaco na Olympique  Lyon pia zinavutiwa  sana na beki huyo wa zamani wa Galatasaray.


Kobbie Mainoo

NAPOLI inataka kusajili kiungo mmoja katika dirisha lijalo la majira ya baridi na chaguo lao la kwanza ni staa wa Manchester United Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 20.


Tetesi za Mainoo kuondoka Man United zimezidi kupamba moto kwa sababu haonekani kuwa na furaha licha ya kocha Ruben Amorim kuendelea kusisitiza kwamba bado anahitaji huduma ya staa huyu katika kikosi chake. Mkataba wake unamalizika 2027.


Santiago Gimenez

STRAIKA wa AC Milan na timu ya taifa ya Mexico, Santiago Gimenez huenda akaondoka katika klabu hiyo katika dirisha lijalo la usajili la Januari na kutimkia England ambako West Ham na Sunderland zimeonyesha nia ya.

Staa huyo, 24,  alionyesha kiwango bora akiwa na Feyenoord mwaka jana kiasi cha kuivutia sana Milan na baadhi ya timu za Ulaya lakini tangu atue katika timu hiyo hajang’ara.


Said el Mala

BRIGHTON inafikiria kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 19, Said el Mala, kutoka Cologne katika dirisha lijalo.Usajili wa fundi huyu unadaiwa kuwa unaweza ukaigharimu Brighton hadi Euro 35 milioni, kiasi ambacho Cologne imegoma kupunguza. Manchester United, Liverpool, na Chelsea pia ni kati ya timu ambazo zinahitaji saini ya fundi huyu.