Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tahadhari kali kwa mashabiki wanaosafiri Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Onyo hilo linakuja wakati maelfu ya mashabiki wa soka wakijiandaa kwenda Marekani na wengine wapo nchini humo kushuhudia mashindano hayo makubwa yanayoanza leo.

WASHINGTON, Marekani: MASHABIKI wa soka watakaosafiri kwenda kushuhudia Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani wametakiwa kubeba pasipoti muda wote kutokana na uwezekano wa kusimamishwa na maofisa wa Uhamiaji wa Marekani (ICE), huku England ikiwaonya raia wake kuwa wasafiri wanapaswa kuwa na nyaraka zinazothibitisha kuwa wanaishi au kutembelea nchi hiyo kihalali.

Onyo hilo linakuja wakati maelfu ya mashabiki wa soka wakijiandaa kwenda Marekani na wengine wapo nchini humo kushuhudia mashindano hayo makubwa yanayoanza leo.

Maofisa wa England wameeleza kuwa kumekuwapo na taarifa mbalimbali katika miezi ya karibuni kuhusu maofisa wa Uhamiaji wa Marekani  kuwakamata baadhi ya watalii kwa ukaguzi wa nyaraka za uhamiaji katika mpango wa serikali ya rais Donald Trump kuwaondoa wahamiaji haramu.

Mbali na Marekani, mashabiki watakaokwenda Mexico kwa ajili ya mechi za Kombe la Dunia pia wamepewa tahadhari kadhaa za kiusalama wakiatakiwa kuacha kuvaa mavazi ya gharama kubwa, vito vya thamani na saa za kifahari ambazo zinaweza kuwavutia wahalifu.

Serikali imeonya kuwa baadhi ya wahalifu huweka dawa za kulevya kwenye vinywaji vya wageni katika baa na migahawa ili kuwaibia au kuwadhuru, huku wakishauriwa kutoacha vyakula au vinywaji bila uangalizi na kuripoti mara moja matukio yoyote yanayotia shaka.

Pia, nchi hiyo imeonya kwamba kumekuwapo na matukio ya watu kuugua au hata kufa ghafla kutokana na matumizi ya pombe zilizochanganywa na kemikali hatari kama methanol, na kuwataka mashabiki kutumia vinywaji kutoka sehemu zinazoaminika na kufuata ushauri wa mamlaka za maeneo husika.

Mashabiki pia wameonywa kuhusu matapeli wanaojifanya maofisa wa polisi pamoja na baadhi ya askari halali wanaodaiwa kuwatoza watalii fedha kwa madai ya makosa madogo au ukiukwaji wa sheria za barabarani, huku wale watakaotumia magari ya kukodi wakielezwa kuwa waangalifu zaidi kwani wamekuwa wakilengwa na wahalifu wanaojifanya maofisa wa usalama ili kupata fedha au mali zao.

England katika taarifa zake pia imekumbusha kuwa uporaji wa vitu vidogo na wizi wa mifukoni ni jambo la kawaida katika maeneo mengi yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na kwenye usafiri wa umma, na kushauri mashabiki kubeba fedha kidogo pamoja na kulinda mizigo hata wanapokuwa hotelini.

Kwa upande wa matumizi ya fedha, wasafiri wameelezwa kuwa waangalifu wanapotumia mashine za ATM au ofisi za kubadilisha fedha, huku mamlaka za Mexico zikipendekeza matumizi ya ATM zilizopo ndani ya maduka makubwa au vituo vya biashara wakati wa mchana ili kupunguza hatari ya kuibiwa.

Hata hivyo, pamoja na tahadhali mbalimbali ambazo kila nchi shiriki ya Kombe la Dunia 2026 imekuwa ikitoa kwa raia wake wanaokwenda Marekani, Canada na Mexico, lakini mataifa hayo waandaji wa fainali hizo yamejipanga vilivyo kuwahakikishia usalama wageni wote kipindi hiki cha mwezi mmoja wa mashindano ikiwamo matumizi ya teknolojia za akili unde (AI) kufuatilia makundi ya uhalifu.

Mathalan, Mexico imeunganisha mifumo yote ya usalama ya polisi na ile ya nyombo vingine vya usalama kunusa matukio hayo kwa kutumia teknolojia hiyo ili kubaini mienendo ya wahalifu na kuchukua hatua kabla hawajatekeleza dhamira zao.

Vilevile, nchi hiyo imeanzisha matumizi ya droni kufuatilia mienendo ya watu wanaohofiwa kujihusisha na uhalifu na pia kuzitumia pale unapojitokea kuhakikisha usalama hasa maisha ya watu yanapokuwa hatarini.

Ndege hizo zitatumia vifaa vya kisasa vya kushambulia na kutoa taarifa za haraka za uokoaji kwa mamlaka husika katika maeneo ambayo yana mazingira magumu.

Ni ndege hizo pia zitatumika katika utoaji wa huduma za dharura za kiafya ndani na nje ya viwanja huko Marekani, lakini kwa Mexico zitatumia pia hata mitaani hasa katika maeneo yenye misongamano mikubwa ya watu.