Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa kasema... Huyu Ni Welbeck Mtupu!

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Huo ni mtazamo wa straika wa zamani wa Watford, Troy Deeney, ambaye bado hajaridhishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden, ambaye alisajiliwa kwa pesa nyingi huko Arsenal kwenye dirisha lililopita akitokea Sporting Lisbon.

LONDON, ENGLAND: KWELI akutukanaye hakuchagulii tusi. Kuna gwiji mmoja wa Ligi Kuu England ameibuka na kudai straika Viktor Gyokeres yupo kwenye viwango sawa na Danny Welbeck na hastahili kuwekwa kwenye kundi la wababe kama Erling Haaland na Harry Kane.

Huo ni mtazamo wa straika wa zamani wa Watford, Troy Deeney, ambaye bado hajaridhishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden, ambaye alisajiliwa kwa pesa nyingi huko Arsenal kwenye dirisha lililopita akitokea Sporting Lisbon.

Kutokana na Kai Havertz kuwa majeruhi, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amelazimika kumtumia straika wake mpya Gyokeres kwenye mechi zao za msimu huu. Na Arsenal imekuwa ikishinda mechi zake ikiwa na huduma ya mshambuliaji huyo uwanjani, hivyo ameongeza kitu kikosini.

Lakini, katika ishu ya kufunga mabao, hilo limekuwa halina mwanzo mzuri kwa Gyokeres.

GYOK 01

Gyokeres amefunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu England, huku moja likiwa la mkwaju wa penalti. Alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini Deeney bado hamwelewi kabisa Gyokeres.

Deeney amesema: “Najaribu kumlinda kwa sababu anacheza vizuri na amefunga mara tatu. Lakini, hawezi kuwa kwenye orodha ya mastraika wa kiwango cha dunia. Hayupo kwenye daraja moja na Haaland na hawezi kuwa kwenye kikapu cha Harry Kane.

“Gyokeres sio straika wa kiwango cha juu, ni mshambuliaji mzuri tu, anacheza vizuri na anafanya vizuri kwa timu yake, lakini ile Arsenal inaweza kufanya vizuri ikiwa na Saka na mabeki wao wawili wa kati. Kwa upande wangu, sioni akileta tofauti. Hana huo uwezo."

GYOK 02

Kwenye ishu ya mabao mangapi atafunga baada ya kutikisa nyavu mara 54 kwenye michuano yote msimu uliopita alipokuwa Sporting Lisbon, Deeney amesema hamtarajii Gyokeres kufunga mara nyingi. Kwa sasa amezidiwa na Welbeck kwenye msimamo wa wafungaji na Deeney hamwoni Gyokeres akifunga mara nyingi kuzidi washambuliaji wengine wa daraja la juu.

“Hawezi kwenda kufunga mara nyingi, nilishasema hilo huko nyuma, sidhani kama atafunga kuwazidi Salah au Isak. Hata sidhani kama atafunga kumzidi Joao Pedro. Ngoja tuone.

“Kwa kifupi tu, Gyokeres kwenye ishu ya kufunga yupo daraja sawa na Danny Welbeck. Na pengine, Welbeck anaweza kufunga zaidi.”

Kuna madai kwamba Gyokeres anafanya vizuri kwa sababu tu Arsenal inafanya vizuri na yeye anatumikia timu hiyo. Lakini, Deeney anaamini kumweka staa huyo kwenye orodha ya mastraika bora, hilo haliko sawa, akisema: “Kama vile ambavyo hajafunga mabao mengi kwenye ligi kumzidi Danny Welbeck. Lakini, ukizungumzia kwenye hilo kwamba hafungi kama Haaland. Utaonekana unamchukia. Lakini, huo ndio ukweli, Welbz amefunga mara nyingi kwenye Ligi Kuu England.” Welbeck, anayekipiga kwenye kikosi cha Brighton, amefunga mabao matano kwenye Ligi Kuu England msimu huu katika mechi tisa alizocheza.