Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Solomon Kalou: Nigeria itatwaa AFCON 2025 kama Ivory Coast itatolewa

KALOU Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, amesema hayo baada ya kipa wa Super Eagles, Stanley Nwabali, kueleza imani yake kuwa Nigeria ina nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa mashindano ya AFCON 2025, ambayo yanaanza kuunguruma nchini Morocco kuanzia Desemba, 21, 2025 na kumalizika Januari 18, 2026.

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Salomon Kalou, amesema ni nchi yake pekee ndiyo inaweza kuizuia Nigeria kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, amesema hayo baada ya kipa wa Super Eagles, Stanley Nwabali, kueleza imani yake kuwa Nigeria ina nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa mashindano ya AFCON 2025, ambayo yanaanza kuunguruma nchini Morocco kuanzia Desemba, 21, 2025 na kumalizika Januari 18, 2026.

Ivory Coast iliifunga Nigeria 2-1 katika mechi ya fainali AFCON 2023 mjini Abidjan na Nwabali amesema kwa sasa Super Eagles ina motisha ya kuleta matokeo bora, kwenye fainali za mwaka huu.

Akijibu maoni ya Nwabali kupitia kituo cha televisheni cha SuperSports, Kalou amesema Super Eagles inaweza kushinda kombe hilo ikiwa tu itakwepa kuikabili Ivory Coast.

“Nigeria inaweza kutwaa ubingwa wa AFCON 2025, lakini hii itategemea kama Ivory Coast, itakuwa imetolewa mapema.”

Akizungumzia ushindi wa Ivory Coast mwaka 2023, Kalou ameongeza: “Ni hisia nzuri kushinda hasa unaposhinda nyumbani, mbele ya watu wako, uwanja mzima, nadhani hakuna hisia zinazoweza kushindana na hizo.

“Unaweza kuuliza mchezaji yeyote aliyecheza kwenye kiwango cha juu, kushinda kwa nchi yako ni kitu tofauti. Haifikii hata hisia za kushinda ukiwa na klabu ambayo inakulipa mshahara mkubwa.”

Katika AFCON 2025, Nigeria imepangwa Kundi C pamoja na Tanzania, Tunisia, na Uganda. Mechi ya kwanza itacheza dhidi ya Tanzania Desemba 23, 2025, kisha itapapatuana na Tunisia Desemba 27, 2025 na mechi ya mwisho ya kundi itakuwa dhidi ya Uganda Desemba 30, 2025.

Ivory Coast imepangwa Kundi F pamoja na Cameroon, Gabon, na Msumbiji. Mechi ya kwanza itacheza dhidi ya Msumbiji Desemba 24, 2025 kisha itakutana na Cameroon Desemba 28, 2025. Mechi ya mwisho ya kundi itakuwa dhidi ya Gabon Desemba 31, 2025.