Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aubameyang atajwa kuikabili Super Eagles mechi ya mchujo Kombe la Dunia 2026

AUBA Pict

Muktasari:

  • Gabon ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25, alama moja nyuma ya Ivory Coast iliyomaliza na pointi 26 na kufuzu moja kwa moja.

Kuelekea mechi muhimu ya mchujo wa Kombe la Dunia la FIFA 2026 dhidi ya Nigeria, Super Eagles, timu ya taifa ya Gabon, inayojulikana kama Panthers, imetangaza kikosi chenye wachezaji 27.

Katika mkutano na wanahabari uliofanyika mjini Libreville, kocha mkuu wa Gabon, Thierry Mouyouma, ametangaza majina ya wachezaji ambao watabeba jukumu la kuivusha nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026, kwa kuhakikisha inaifunga Nigeria.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa, itafanyika Alhamisi, Novemba 13, 2025, kwenye Uwanja wa C.S. Prince Héritier Moulay El Hassan, uliopo Rabat, Morocco. 

Mshindi kati ya Gabon na Nigeria atachuana na mshindi kati ya Cameroon na DR Congo katika hatua inayofuata ya mchujo wa Afrika.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye kwa sasa anachezea Marseille ya Ufaransa, ataongoza safu ya ushambuliaji ya Gabon katika mechi hiyo. 

Mbali mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36, wachezaji wengine wazoefu walioitwa na kocha Mouyouma ni Mario Lemina, Noha Lemina na Denis Bouanga, ambaye ni mfungaji bora wa Gabon kwenye hatua ya kufuzu akiwa na mabao manane.

Orodha kamili ya kikosi cha The Panthers:

Makipa.
Jean-Noël Amonome (AS Arta/Solar7, Djibouti), Donald Nzé (AS Mangasport), Anthony Mfa Mezui (FC Rodange, Luxembourg)

Mabeki.
Bruno Ecuele Manga (Chamois Niortais, Ufaransa), Lloyd Palun (RWD Molenbeek, Ubelgiji), Aaron Appindangoye (Hana Klabu), Johann Obiang (Stade Lavallois, Ufaransa), David Sambissa (Pau FC, Ufaransa), Sidney Obissa (Olympiakos Nicosia, Cyprus)

Viungo.
Mario Lemina (Wolverhampton Wanderers, England), Guélor Kanga (Red Star Belgrade, Serbia), Jim Allevinah (Clermont Foot, Ufaransa), Louis Ameka Autchanga (Sabah FC, Azerbaijan), Noha Lemina (Yverdon Sport FC, Uswisi), Yoann Wachter (US Saint-Malo, Ufaransa)

Washambuliaji.
Pierre-Emerick Aubameyang (Marseille, Ufaransa), Denis Bouanga (Los Angeles FC, Marekani), Axel Meye (CR Belouizdad, Algeria), Aaron Boupendza (Al-Shabab, Saudi Arabia), Ulrick Eneme Ella (Angers SCO, Ufaransa).

Ingawa Gabon ilicheza vizuri katika hatua ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026, haikuweza kuipiku Ivory Coast ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika Kundi E.

Gabon ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25, alama moja nyuma ya Ivory Coast iliyomaliza na pointi 26 na kufuzu moja kwa moja.