Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bambucha alikimbiwa na mwanamke kisa funza

KAMERA Pict


KABLA ya kupata hitilafu katika mwili wake na jina lake kuwa juu enzi hizo wakati anatamba katika filamu mbalimbali nchini, msanii Omary Babuu 'Bambucha' mapenzi yake na aliyekuwa mkewe yalikuwa mfano wa kuigwa na jamii iliyokuwa inawazunguka na baadhi yao waliitamani kapo yao.


Ilipomfikia zamu ya upande wa pili wa mapenzi kugeuka kuwa shubiri, anasimulia ilivyomchukua muda kukubaliana na hali na kuanza safari mpya ya upweke kwa muda.


Katika mahojiano yake na Nyuma ya Kamera wiki hii, anasimulia kisa kilichofanya akimbiwe na mkewe huyo ambaye alibahatika kupata naye watoto wawili, ambao ndio ilikuwa faraja yake ya kuamini mwanzo mpya wa malezi ya mzazi mmoja (single father).

Anasema alipata changamoto ya ugonjwa wa sukari, baada ya kutokwa vidonda na kuanza kunuka na kutoa funza aliyekuwa mkewe huyo aliyezaa naye watoto wawili, Said na Ozil alimkimbia na kuwaacha vijana wake wakiwa wadogo.

KAME 01

"Mwanamke wangu alishindwa kuvumilia harufu mbaya ya mguu na mafunza yaliyokuwa yananitoka, akaondoka na kwenda kuolewa na tajiri, lakini hawakufunga ndoa alipokufa kwa figo huyo mwanaume hakuna alichoambulia alirudi kwao, kwa sasa ananipigia simu namwambia utawaona wanao lakini mapenzi yalishakufa," anasema Bambucha na kuongeza;

"Nakumbuka kijana wangu mdogo alikuwa ananiambia baba usife tutateseka, sisi tutakuwa tutakutunza utakuwa na furaha, hilo lilikuwa linanifanya nipate nguvu ya kuanza maisha mapya na wanangu ambao ndio walikuwa faraja pekee ya maisha yangu.

"Kwa namna nilivyokuwa nampenda mwanamke wangu hiyo ikawa sababu ya kijana wangu kumpa jina la Ozil, wakati ana mimba yake alikuwa anampenda Mesut Ozil, mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Arsenal."

KAME 02

Je, hali yake kimahusiano wakati kakimbiwa na mke ilikuwaje. Anaeleza:"Nilikutana na mdada mmoja alikuwa ananisaidia na kunihudumia, nikajikuta nimeingia naye katika mahusiano mara akapata mimba wazazi wake walipokuwa wamesikia walimchukua, hivyo namtunza mtoto wangu.

Anaongeza:"DM yangu inafuatwa na wanawake matajiri wenye magari na nyumba, mapenzi yana nguvu sitaki kuwaacha watoto wangu, ambao kila wakati wananiambia baba wewe ni kila kitu kwetu, japokuwa gari langu kwa sasa ni baiskeli ya matairi matatu nina amani nalo.

"Naishi kwa mama yangu mdogo naye ni mtu mzima kwa sasa, kipato changu kinatokana na dawa ninazotengeneza za sukari pamoja na sabuni za mchele ambazo ni nzuri kwa ngozi.

KAME 03

"Kuna mzungu mmoja yupo Ujerumani aliguswa baada ya kuona video zangu akanipa pesa za kununulia mashine ya kutengenezea sabuni za mchele na akanifundisha jinsi ya kutengeneza, kwa sasa napata pesa za kubadilisha mboga kwa ajili ya familia yangu"

Anasisitiza mapenzi hayana fomula na yanaleta upofu wa kutojua machungu yake kipindi ambacho unakuwa na raha, kikubwa kwa wanaume wakipata watu wenye upendo wa kweli bila kuangalia unachomiliki ndivyo bora zaidi.

"Sisi wanaume kuna wakati tunaangalia sana vitu vya nje, ila kusema ukweli kupata mwanamke mwenye upendo wa kweli huo ni utajiri tosha wa utulivu wa mwanaume," anasema.