Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siondoki! Bruno Fernandes amaliza utata Man United

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Manchester United dirisha hili la usajili, huku Al-Nassr inayommiliki nyota Cristiano Ronaldo ikitajwa kuwa miongoni mwa timu zinazomuwania kwa nguvu.

MANCHESTER, ENGLAND: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameripotiwa kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake kwa kuamua kubaki Old Trafford kwa angalau msimu mmoja zaidi licha ya kuendelea kuwindwa na klabu kadhaa za Saudi Arabia.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Manchester United dirisha hili la usajili, huku Al-Nassr inayommiliki nyota Cristiano Ronaldo ikitajwa kuwa miongoni mwa timu zinazomuwania kwa nguvu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Fernandes tayari amewaambia baadhi ya wachezaji wenzake pamoja na watu wake wa karibu hana mpango wa kuondoka Manchester kwa sasa.

BRU 03

Nyota huyo, 31, anaendelea kuwa sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya Manchester United, huku viongozi wa klabu hiyo wakionekana kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusu hatma yake.

Fernandes bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa, huku Manchester United ikiwa na chaguo la kuongeza mmoja zaidi. Pia, mkataba wake una kipengele cha kuondoka kwa Euro 65 milioni kwa klabu zisizo za England.

Licha ya uamuzi huo, klabu za Saudi Arabia bado hazijakata tamaa. Al-Hilal, Al-Nassr na Al-Ittihad zote ziliwasiliana na mchezaji huyo dirisha la usajili lililopita, huku Al-Hilal ikielezwa kuwa karibu zaidi kumpata kabla ya mchezaji huyo kubadilisha msimamo wake.

BRU 02

Inaelezwa Al-Nassr bado ina nia ya kumshawishi Fernandes kujiunga na klabu hiyo ili kuunda upya ushirikiano wake na nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo.

Tetesi hizo zimeongezeka zaidi baada ya kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Roberto Martinez kuripotiwa kuwa katika mazungumzo ya kuinoa Al-Nassr baada ya Kombe la Dunia.

Mustakabali wa Fernandes uliwahi kuwa na sintofahamu baada ya nyota huyo kudai katika mahojiano viongozi wa Man United walikuwa tayari kumuachia aondoke kama angeamua kufanya hivyo.

“Klabu ilitaka niondoke. Niliwaambia viongozi kuhusu hilo, lakini nafikiri hawakuwa na ujasiri wa kufanya uamuzi huo kwa sababu kocha alitaka nibaki,” aliwahi kusema Fernandes.

BRU 01

Hata hivyo, hali imebadilika ndani ya Manchester United, huku Kocha Michael Carrick akisisitiza umuhimu wa kumhifadhi nahodha huyo kama sehemu ya msingi ya kikosi chake.

Tangu alipojiunga na Manchester United akitokea Sporting CP Januari 2020, Fernandes amekuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa klabu hiyo. Amefunga mabao 107 na kutoa pasi 108 za mabao katika mechi 327 alizoichezea timu hiyo.

Msimu uliopita aliweka rekodi mpya ya Ligi Kuu England kwa kutoa pasi 21 za mabao, akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa pamoja na Thierry Henry na Kevin De Bruyne.

Ubora wake umeendelea hata katika Kombe la Dunia la mwaka huu na alitoa pasi ya bao katika ushindi wa mabao 5-0 wa Ureno dhidi ya Uzbekistan.