Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku ya kwanza kazini halafu ni mbaya

Muktasari:

  • Kwenye mchezo huo, Khusanov alifanya makosa ya kumruhusu Nicolas Jackson kuruka juu kupiga mpira kichwa na kumtengenezea Noni Madueke na kufunga bao Chelsea. Bahati nzuri kwake, Man City ilishinda 3-1.

LONDON, ENGLAND: SIKU yako ya kwanza kazini na kisha mambo yanakwenda kombo ni jambo litakalobaki kwenye kumbukumbu zako maisha yote. Kitu hicho, muulize staa mpya wa Manchester City, Abdukodir Khusanov, ambaye Jumamosi iliyopita aliichezea mechi ya kwanza timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea.

Kwenye mchezo huo, Khusanov alifanya makosa ya kumruhusu Nicolas Jackson kuruka juu kupiga mpira kichwa na kumtengenezea Noni Madueke na kufunga bao Chelsea. Bahati nzuri kwake, Man City ilishinda 3-1.

Hata hivyo, kwenye soka Khusanov si mchezaji wa kwanza kuwa na siku mbaya kwenye mechi yake ya kwanza katika klabu yake baada ya kuwapo wengine kibao.


Moises Caicedo vs West Ham

Chelsea ilivunja rekodi ya uhamisho England wakati ilipomsajili kiungo Caicedo kwa ada ya Pauni 115 milioni.

Wakati wengi wakiamini kiungo huyo atafanya mambo makubwa kuendana na thamani yake ya pesa, Caicedo hakuwa na wakati mzuri katika mechi yake ya kwanza dhidi ya West Ham United na aliingia kutokea benchini. Katika mechi hiyo, Caicedo alifanya makosa mengi ikiwamo kusababisha penalti kwenye kipigo cha mabao 3-1.


Lionel Messi vs Hungary

Hakuna ubishi, Messi ni mwanasoka bora wa muda wote baada ya kuingoza Argentina kunyakua taji la Kombe la Dunia 2022 – lakini mechi yake ya kwanza kwenye soka la kimataifa, kazini kwake palikuwa na kazi.

Fowadi huyo mechi yake ya kwanza kuichezea Argentina ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Hungary na aliingia kutokea benchini kwenye dakika ya 63.

Hata hivyo, mambo hayakuwa mazuri na Messi alidumu kwa dakika mbili tu uwanjani na kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Vilmos Vanczak.


Thiago Silva vs West Brom

Thiago Silva alikuwa moja ya usajili bora kabisa kwenye kikosi cha Chelsea katika zama za sasa, lakini soka la Ligi Kuu England lilikuwa mtihani mzito kwa Mbrazili huyo mwanzoni mwa maisha yake.

Katika mechi ya ugenini dhidi ya West Brom, ambayo ilikuwa ya kwanza kwa Mbrazili huyo kuichezea Chelsea, alipoteza mpira akiwa karibu na goli lake na hivyo kumruhusu Callum Robinson kufunga bao la pili kati ya matatu ya West Brom waliyofunga kwenye kipindi cha kwanza. Alishindwa kuwakaba wachezaji wa timu pinzani.


Patrice Evra vs Man City

Evra alijiunga na Manchester United, Januari 2006 na alikwenda kufurahia maisha yake bora kabisa huko Old Trafford, akishinda mataji 14 – ikiwamo matano ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akichezea timu hiyo mara 379.

Lakini, mambo yake hayakuwa mazuri kabisa kwenye mechi yake ya kwanza Man United na alitolewa kwenye kipindi cha kwanza tu, baada ya kucheza dakika 45 na alikuwa na wakati mgumu kuburuzwa na Trevor Sinclair. Kocha Sir Alex Ferguson alishindwa kuvumilia na kumtoa katika mechi hiyo ya kipigo kutoka kwa Man City.


Joe Cole vs Arsenal

Kiungo mshambuliaji, Joe Cole alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi yake ya kwanza kuitumikia Liverpool na kufanya mambo kuwa mabaya kabisa katika mwanzo wake wa maisha huko Anfield.

Mechi ya kwanza ya Cole ilikuwa chini ya Arsenal mwaka 2010 na hakika baada ya hapo, mambo yalikwenda kombo kwa kiungo Cole na hakuwa na uhusiano mzuri kabisa na mashabiki wa Anfield.


Gervinho vs Newcastle

Wakati Arsenal ilipomsajili Gervinho kutoka Lille mwaka 2011, baada ya kuhusushwa na aliyekuwa mchezaji mwenzake wakati huo Eden Hazard, ambaye alinaswa na Chelsea, mashabiki wa Arsenal walikuwa na matumaini makubwa winga huyo atakwenda kuwa balaa zito kwenye kikosi chao kama ilivyo kwa Mbelgiji huyo. Lakini, mambo yalitibuka kwenye mechi ya kwanza tu ya mchezaji Gervinho na alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchapa kibao Joey Barton katika mechi ya sare bila kufungana dhidi ya Newcastle.


Saul Niguez vs Aston Villa

Licha ya kwamba hakuwa na wakati mzuri chini ya Kocha Diego Simeone, kiungo Saul bado alikuwa akihesabika kama mmoja wa wachezaji mahiri kabisa barani Ulaya wakati alipokuwa akijiunga kwa mkopo huko Chelsea akitokea Atletico Madrid mwaka 2021. Lakini, kwenye mechi yake ya kwanza aliteswa sana na John McGinn kwenye safu ya kiungo na alipiga pasi za hovyo ndani ya uwanja na kujiweka kwenye wakati mgumu kwelikweli katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Aston Villa.


Rio Ferdinand vs Leicester City

Leeds United iliweka rekodi Uingereza wakati iliposajili Ferdinand na kumfanya kuwa beki ghali duniani ilipolipa Pauni 18 milioni kupata saini yake huko Elland Road akitokea West Ham United mwaka 2000.

Lakini, klabu yake mpya ya Leeds ilikuwa na wakati mgumu kwenye mechi ya kwanza tu kwake na Kocha David O’Leary alihitaji kuwa na nguvu mpya kwenye safu ya linzani, lakini mambo yalikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kuwa nyuma kwa mabao matatu mbele ya Leicester City baada ya dakika 28 tu. Leeds iliruhusu mabao ya Robbie Savage, Ade Akinbiyi na Gerry Taggart.


Wayne Bridge vs Arsenal

Ikiwa kwenye vita ya kupambana isishuke daraja mwanzoni mwa mwaka 2011, West Ham United ilifanya usajili wa kumnasa mmoja wa mabeki wenye uzoefu Wayne Bridge wakiamini watakwenda kuimarisha safu yao ya ulinzi na kuwaweka kwenye hali ya usalama.

Lakini, kwenye mechi yake ya kwanza tu imekuwa mbaya kwake na alifanya makosa yaliyowaruhusu Arsenal kufunga mara nyingi kwenye mchezo huo.

Hilo pekee likiwa halitoshi, alisababisha penalti pia kwenye dakika za mwisho na kuifanya Arsenal kupata ushindi wa mabao 3-0.

West Ham iliporomoka hadi nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.


Alex Jankewitz vs Man United

Kama kuna watu walikuwa na siku mbaya kazini kwenye siku yao ya kwanza badi Alex Jankewitz ni namba moja baada ya kudumu kwa sekunde 79 tu uwanjani kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Southampton.

Mechi hiyo ilikuwa chini ya Manchester United, na ilichapwa Februari 2021.

Mchezaji huyo alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Scott McTominay. Mechi hiyo ilimalizika kwa Southampton kukutana na kipigo cha mabao 9-0. Jankewitz hakucheza tena mechi nyingine katika timu hiyo na aliuzwa kwenda Young Boys msimu ulipomalizika.