Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SENEGAL YAMCHAPA BINGWA AFRIKA KIKAPU

SENEGAL Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Dakar Arena usiku wa kuamkia leo Jumapili, Agosti 30, ulikuwa wa ushindani mkali hadi dakika za mwisho, kabla Senegal kuibuka na ushindi huo mwembamba mbele ya mashabiki wake.

DAKAR, SENEGAL: Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Senegal imepata ushindi wa kihistoria wa pointi 84-82 dhidi ya mabingwa wa Afrika, Angola, katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu 2027.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Dakar Arena usiku wa kuamkia leo Jumapili, Agosti 30, ulikuwa wa ushindani mkali hadi dakika za mwisho, kabla Senegal kuibuka na ushindi huo mwembamba mbele ya mashabiki wake.

Brancou Badio alikuwa miongoni mwa nyota walioibeba Senegal katika mchezo huo, huku ushindi huo ukiwa kama kisasi baada ya matokeo ya michezo iliyopita kati ya timu hizo.

Matokeo hayo yameipa Senegal nafasi nzuri katika mbio za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za FIBA 2027 zitakazofanyika nchini Qatar, huku ushindani wa kuwania nafasi za Afrika ukiendelea kupamba moto.

Afrika itapata nafasi tano katika Fainali hizo, huku tiketi hizo zikitolewa kupitia hatua ya kufuzu inayoendelea.

Kwa mujibu wa mfumo wa kufuzu, timu mbili za kwanza kutoka kila Kundi E na F zitafuzu moja kwa moja, huku nafasi ya tano ikienda kwa timu itakayomaliza ikiwa na rekodi bora zaidi kati ya zitakazoshika nafasi ya tatu katika makundi hayo mawili.

Baada ya matokeo hayo, Ivory Coast inaongoza Kundi F ikiwa na pointi 15, ikifuatiwa na Senegal yenye pointi 14. Mali pia ina pointi 14 katika nafasi ya tatu, lakini inazidiwa na Senegal kwa wastani wa vikapu.

Angola iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 13, ikifuatiwa na Misri yenye pointi 12, huku DR Congo ikiwa mkiani kwa pointi 10.

Katika Kundi E, Cameroon inaongoza ikiwa na pointi 15, ikifuatiwa na Sudan Kusini yenye pointi 14.

Tunisia iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13, sawa na Guinea inayoshika nafasi ya nne, huku Nigeria ikiwa ya tano kwa pointi 12 na Cape Verde ikifunga kundi kwa pointi 11.