Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katwila aanza majigambo

Muktasari:

  • Kauli ya Katwila inajiri baada ya timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026, tangu iliposhuka daraja msimu wa 2023-2024, kucheza mechi mbili kati ya nne hadi sasa kwenye Uwanja wa Bukombe na kushinda moja na kutoka sare moja.

BAADA ya kupata pointi nne katika mechi mbili za nyumbani, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila amesema malengo ya timu hiyo kwa sasa ni kuhakikisha Uwanja wa Bukombe unakuwa ni mwiba mkali kwa wapinzani wote watakaoenda kucheza nao.

Kauli ya Katwila inajiri baada ya timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026, tangu iliposhuka daraja msimu wa 2023-2024, kucheza mechi mbili kati ya nne hadi sasa kwenye Uwanja wa Bukombe na kushinda moja na kutoka sare moja.

Timu hiyo inayotumia Uwanja wa Bukombe uliopo mji mdogo wa Ushirombo, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, ilianza kuifunga Kagera Sugar mabao 6-2, Agosti 22, 2026, kisha sare ya 2-2, dhidi ya Azam FC, Agosti 28, 2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katwila alisema kupata pointi nne nyumbani katika mechi mbili sio jam-bo dogo kutokana na aina ya wapinzani waliocheza nao, ingawa mwenendo huo wa kuridhisha una-wajenga wachezaji vizuri kisaikolojia ili kupambana.

“Ushindani ni mkubwa sana kwa sababu hata mechi yetu na Azam FC ilikuwa ni ngumu kuamini tuta-sawazisha na kupata pointi moja, kwetu imetuongezea morali ya kupambana na kuhakikisha uwanjani kwetu sio rafiki kwa wapinzani,” alisema Katwila.

Aidha, Katwila alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wachezaji kwa ukomavu mkubwa waliouonyesha hadi sasa, huku akiwataka kuendelea kupambana kwa ajili ya mashabiki wa Mkoa wa Geita, ambao wame-beba matumaini makubwa kwao ya Kanda ya Ziwa.

Katika mechi nne ilizocheza Geita ilianza kwa ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Mbeya City, Agosti 14, 2026, ikachapwa 1-0 na Namungo FC, Agosti 18, 2026, ikaifunga Kagera Sugar mabao 6-2, Agosti 22, 2026 na sare ya 2-2 na Azam, Agosti 28, 2026.