Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Yanga, Barker ‘awawashia moto’ Simba

KOCHA wa Simba, Steven Barker amewapa kazi maalum mastaa wa kikosi hicho ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuifanya timu yake inufaike zaidi katika dakika 90 za kila mechi, huku akiwataka kutumia kila nafasi wanayoipata.

Simba imeshacheza mechi nne za Ligi Kuu Bara, imeshinda tatu ugenini na moja nyumbani na ilianza kwa kuifunga mabao 2-0 Kagera, ikiaichapa Pamba Jiji 2-1, na Singida Black Stars 2-1 zikiwa ni za ugenini.

Hata hivyo, juzi mashabiki wa timu hiyo hawakuridhishwa na kiwango cha timu ilipovaana na Coastal Union na kushinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Meja Usamhyo, Mbweni, kutokana na mastaa wake kushindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi walizopata.

Katika mazoezi ya timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, nyuma ya Yanga kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, juzi kocha huyo alionyesha kutaka mabadiliko katika kikosi chake kabla ya mechi ya ligi dhidi ya Geita Gold na ile ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, Jumapili ijayo.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kabla ya mazoezi, Barker ambaye alionekana kuwa mkali kuli-ko siku zote, alisema hakuridhishwa na kiwango cha timu hiyo dhidi ya Coastal Union na walishindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga ambazo zingeweza kuwasaidia kupata ushindi mnono.

“Kocha amesema hakuridhishwa na kiwango cha timu pamoja na tulishinda. Anaamini tulikuwa tuna-weza kupata mabao mengi zaidi katika mchezo huo na kutuweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

“Kwa sasa mpinzani wetu yupo juu kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Kama tungetumia vizuri nafasi tulizopata, basi tungekuwa katika nafasi nzuri zaidi kwa sasa.

“Mbali na hilo, kocha alitoa mwongozo mpya kwenye kikosi chake, kuna matukio ambayo akiwa benchi hayaonekani vizuri uwanjani, hivyo benchi linaweza kushindwa kufahamu kama tukio fulani lilikuwa faulo au la.

“Amewataka wachezaji kuonyesha ishara benchi wanapoamini tukio alilofanyiwa mchezaji wa Simba linahitaji marejeo ya Football Video Support (FVS) au linapaswa kuachwa liendelee.

Amesema kila timu inapewa kadi mbili tu za marejeo, hivyo zikitumika vibaya, kuna wakati timu inawe-za kukosa haki yake. Ni jukumu la wachezaji kuhakikisha wanatoa ishara kwa viongozi wa benchi ili kadi hizo zitumike vizuri na kuepuka hali iliyotokea kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union na benchi liliom-ba marejeo likidhani tukio la madhambi aliyofanyiwa Elie Mpanzu lilistahili penalti, kumbe halikuwa hivyo,”   kilisema chanzo hicho kutoka kikosi cha Simba.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kocha huyo ameweka wazi Simba itacheza kwa mfumo tofauti kabisa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kuwa tayari wamewasoma wapinzani wao na kufahamu ubora pamoja na udhaifu wao.

Simba inarejea uwanjani kesho kuvaana na Geita Gold katika mchezo wa tano wa Ligi Kuu Bara uta-kaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 12:00 jioni. Baada ya mchezo huo, timu hiyo itaanza maandalizi kwa ajili ya michuano ya CAF.