Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Yanga amuibua kocha Msenegal

Muktasari:

  • Cheikh Ibrahima Touré (29) ni mshambuliaji wa Yanga aliyesajiliwa Julai 2026, kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili akiwa ameshafunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao. Ana asili ya Senegal na Ufaransa.

KIWANGO cha mshambuliaji wa Yanga, Cheikh Toure kimemuibua kocha wa zamani wa Azam FC, Yusuf Dabo, huku akimpa mbinu ya jinsi anavyotakiwa kucheza ili aweze kutoboa katika soka la hapa Bongo.

Cheikh Ibrahima Touré (29) ni mshambuliaji wa Yanga aliyesajiliwa Julai 2026, kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili akiwa ameshafunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao. Ana asili ya Senegal na Ufaransa.

Alitua Yanga akitokea Al-Jabalain FC ya Saudi Arabia. Akiacha rekodi ya kuwa na msimu bora zaidi na alicheza mechi 34, akafunga mabao 19 na kupiga asisti 5.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dabo ambaye anayafahamu vizuri mazingira ya soka la Tanzania baada ya kufanya kazi Azam, alisema anaamini Toure ana uwezo mkubwa, lakini anatakiwa kuongeza nguvu na kujiandaa kwa aina ya ushindani uliopo katika Ligi Kuu Bara.

“Namfahamu vizuri Toure na najua ana ubora wake, lakini anatakiwa kujiandaa sana kiushindani kwa sababu Ligi ya Tanzania si rahisi. Hapa unahitaji kuwa tayari kupambana kwa nguvu na kutumia uwezo wako katika mazingira yenye ushindani mkubwa,” alisema Dabo.

Msenegali huyo alisema soka la Tanzania linahitaji wachezaji kuwa imara kimwili kutokana na namna ambavyo mechi zinavyochezwa, huku washambuliaji wakikutana na mabeki wanaowalazimisha ku-tumia nguvu katika kutafuta nafasi za kufunga.

“Anatakiwa kujiimarisha kwa nguvu. Soka la Tanzania linahitaji matumizi mengi ya nguvu. Kama mshambuliaji unapaswa kuwa tayari kupambana na mabeki, kulinda mpira na kutafuta nafasi hata un-apobanwa,” alisema.

Dabo alitoa mfano wa baadhi ya washambuliaji waliowahi kuwasili Azam kutoka Amerika, ambao licha ya kuwa na viwango vizuri, walipata changamoto kufanya vizuri kutokana na kushindwa kuhimili mahitaji ya soka la Tanzania.

“Nilipokuwa Azam walikuja washambuliaji wazuri kutoka Amerika. Walikuwa na uwezo mzuri wa ku-cheza mpira, lakini walishindwa kufanya vizuri kwa sababu walipata ugumu kuhimili mahitaji ya nguvu yaliyopo kwenye ligi yetu,” alisema.

Aliongeza, Toure amefanya uamuzi wa kujiunga na moja ya timu zenye presha kubwa zaidi ya matokeo nchini, hivyo anatakiwa kuwa tayari kubeba matarajio ya mashabiki wa Yanga.

“Yanga ni timu yenye presha kubwa ya matokeo. Huko mashabiki wanataka kuona ushindi na mabao. Lakini namjua Toure, akianza kufunga tu, mashabiki watafurahia uwezo wake na kila kitu kitabadilika,” alisema Dabo.

Toure ambaye anavalia jezi namba tisa, kabla ya Yanga kucheza dhidi ya Pamba Jiji, alicheza dhidi ya Namungo (dakika 46), Coastal Union (dakika 27) na JKT Tanzania (dakika 22) na hakufunga katika mechi hizo.