Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare ya Arsenal yamuibua Guardiola, arusha kijembe

GUARDIOLA Pict

Muktasari:

  • Arsenal ilikaribia kushinda mechi hiyo, baada ya kuongoza kwa 1-2, lakini Brian Brobbey aliharibu mpango huo kwa kuifungia Sunderland bao la kusawazisha katika dakika ya 90+4.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola, ameipiga kijembe Arsenal, baada ya kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya Sunderland iliyokuwa nyumbani Stadium of Light, jana Jumamosi, Novemba 08, 2025.

Arsenal ilikaribia kushinda mechi hiyo, baada ya kuongoza kwa 1-2, lakini Brian Brobbey aliharibu mpango huo kwa kuifungia Sunderland bao la kusawazisha katika dakika ya 90+4.

Akizungumza kuelekea mechi ya EPL dhidi ya Liverpool, kocha wa Man City Guardiola amesema Arsenal inatakiwa kutambua kuwa, sio klabu bingwa katika Ligi ya EPL, hivyo wajitulize.

Guardiola amesema bado mbio za ubingwa zinaelndelea na ndio maana kilichotokea kwenye mechi ya jana ya Arsenal, kimempa jambo la kuzungumza na kuikumbusha klabu hiyo ya kaskazini mwa London kuwa sio mabingwa.

Ingawa Guardiola amekiri kwamba Arsenal inaonekana kuwa na kikosi imara na cha kushangaza msimu huu, lakini amesisitiza mwisho wa msimu itadhihirika kama inaweza kufanya jambo na kuwa bingwa.

GUAD 01

“Leo Jumapili tunacheza dhidi ya Liverpool, ninakiri kusema kuwa, tutacheza na mabingwa wa EPL, lakini Arsenal sio bingwa kwa sasa,” amesema Guardiola.

“Arsenal si mabingwa, mabingwa ni Liverpool. Wanakuja Etihad kutetea taji lao, kwa hiyo ndugu zetu wa London wajitulize kwa sasa, japo wana kikosi imara na cha kushangaza.

“Nina nafasi ya kujipima kwa mabingwa watetezi, ili mwisho wa msimu tufahamu nini tutakachokipata, ninaamini katika kiwango cha wachezaji wangu kwa sasa, hivyo tutapambana na kusaka ushindi dhidi ya Liverpool,” amesema Guardiola.

Hata hivyo, Arsenal inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi ya EPL kwa pengo la pointi saba dhidi ya Man City na pointi nane dhidi ya Liverpool, ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo.