Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola ammisi Jurgen Klopp EPL

Muktasari:

  • Mechi hiyo itakuwa ya 1000 kwa Guardiola katika kazi yake ya ukocha, lakini kubwa akikumbuka upinzani aliokuwa nao dhidi ya Klopp kwa nyakati mbili tofauti walizowahi kuwa kwenye ligi moja.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA, Pep Guardiola amekiri “amemmisi Jurgen Klopp” wakati chama lake likijiandaa kukabiliana na Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uwanjani Etihad, Jumapili.

Mechi hiyo itakuwa ya 1000 kwa Guardiola katika kazi yake ya ukocha, lakini kubwa akikumbuka upinzani aliokuwa nao dhidi ya Klopp kwa nyakati mbili tofauti walizowahi kuwa kwenye ligi moja.

Mpinzani wa nguvu wa Guardiola kwenye Ligi Kuu England alikuwa Klopp na kikosi chake cha Liverpool, ambaye walichuana kwenye mbio za ubingwa hadi dakika za mwisho kabisa kwenye msimu mara mbili tofauti, huku misimu mingine vita ilikuwa ni vuta nikuvute.

Kabla ya makocha hao wawili kuonyeshana ubabe kwenye Ligi Kuu England walianzia huko Ujerumani kwenye Bundesliga, wakati mmoja alipokuwa Bayern Munich na mwingine Borussia Dortmund.

Kipindi hicho Klopp alikuwa Dortmund na Guardiola alikuwa kwenye kikosi cha Bayern na vita yao ilihamia kwenye Ligi Kuu England na kuonyeshana ubabe.

Wengi wanaamini vita ya makocha hao ilifanya Ligi Kuu England kuwa na upinzani mkali katika mbio za ubingwa, lakini sasa Man City ya Guardiola itakwenda kukumbana na Liverpool, Jumapili huku kukiwa na kocha mwingine, Mdachi, Arne Slot.

Guardiola alisema: “Kama tutachangia mpinzani mmoja katika muda wako wote, ningeweza kutaja wengi, nimekuwa muda mrefu kwenye hii nchi. Lakini, Liverpool, hasa kipindi cha Jurgen, walikuwa wapinzani wangu wakubwa kwenye hii nchini.”

Katika msimu wa mwisho uliowakutanisha makocha hao Guardiola na Klopp, hakukuwa na mbeba. Timu zao zilitoka sare ya 1-1 uwanjani Etihad na ilirudia matokeo hayo katika mechi nyingine iliyofanyika Anfield.

Makocha hao kila mmoja alipata wakati wa kushinda dhidi ya mwenzake na vita yao ilikuwa ya uwanjani zaidi na nje ya uwanjani kulikuwa na heshima kubwa baina yao.

Tangu alipoanza kazi ya kuinoa Barcelona B 2007, Guardiola ameshuhudia mechi 999 akiwa kwenye benchi la ufundi, ameshinda 715 kati ya hizo.