Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saluti! Liverpool yastaafisha jezi ya Diogo Jota

Muktasari:

  • Ulimwengu wa wapenda soka bado unaomboleza msiba wa mkali huyo wa kimataifa wa Ureno, ambaye alikuwa kipenzi cha wengi huko Anfield.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imeamua kuistaafisha jezi Namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na mshambuliaji Diogo Jota ikiwa ni heshima ya kipekee kwa staa huyo wa Ureno aliyefariki dunia kwenye ajali ya gari huko Hispania wiki iliyopita akiwa na mdogo wake, Andre Silva.

Ulimwengu wa wapenda soka bado unaomboleza msiba wa mkali huyo wa kimataifa wa Ureno, ambaye alikuwa kipenzi cha wengi huko Anfield.

Katika kutukuza heshima ya staa huyo, Liverpool imestaafisha jezi Namba 20 katika ngazi zote.

Taarifa ya klabu ilisomeka hivi: “Baada ya kushauriana na mke wake, mrembo Rute na familia yake, klabu inapenda kutangaza jezi Namba 20 itastaafishwa kwa ajili ya heshima na kumbukumbu ya Diogo na hilo litakuwa kwenye ngazi zote, ikiwao timu ya wanawake na kwenye akademia.

“Na hilo si kwa sababu ya mchango wake aliotoa uwanjani akiwa na kikosi chetu, bali ni ushirikiano, utu na hekima kubwa aliyokuwa amewapa wachezaji wenzake, mashabiki na watu wengine wote katika kuhakikisha kunakuwa na muunganiko mzuri katika ujenzi wa timu.”

Mabosi wa Liverpool hawakutaka kustaafisha jezi hiyo ya Jota kwenye kikosi chao bila ya kupata ushauri kutoka kwa mkewe, mrembo Rute pamoja na wanafamilia wengine.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa FSG, Michael Edwards alisema: “Kama klabu, tulikuwa na ufahamu mzuri wa kuhusu mashabiki wetu na namna ambayo tumeguswa na hili jambo. Kulikuwa na umuhimu mkubwa wa kumshirikisha mke wa Diogo, Rute na familia yake juu ya uamuzi wetu ili kuwafanya kuwa watu wa kwanza kufahamu dhamira yetu.

“Naamini hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya Liverpool Football Club kutoa heshima ya aina hiyo kwa mchezaji mmoja. Hivyo, hiyo ni heshima ya kipekee kwa mtu wa kipekee. Kwa kustaafisha jezi yake, hii inafanya jambo kuwa la kudumu na halitasahaulika.

“Diogo alijiunga na sisi 2020, alikuwa akivaa Namba 20 na ameivaa kwa heshima na viwango vyote. Na kwa heshima kubwa ya klabu, daima yeye atakuwa Namba 20 wetu.”

Tukio hilo lilikwenda sambamba na hafla fupi ya kufanya kumbukumbu ya kipekee ya kuweka maua uwanjani Anfield, kwenye tukio lililomhusisha pia mke wake Jota, mrembo Rute Cardoso, ambaye aliambatana na watoto wake kuweka mashada ya maua, skafu uwanjani hapo.

Mastaa wa Liverpool, Virgil van Dijk, Joe Gomez na Darwin Nunez waliokuwa miongoni waliohudhuria tukio hilo, sambamba na kocha wao, Arne Slot.

Jota, 28, ambaye ni baba wa watoto watatu alifariki dunia ajalini akiwa na mdogo wake, wakati gari yao waliokuwa wakisafiria Lamborghini kupasuka tairi moja na kuwaka moto huko Hispania wakati walipokuwa wakiwahi kivuko cha kuwaleta England.

Alifunga pingu za maisha na mrembo Rute siku 11 kabla ya ajali hiyo. Taarifa ya polisi ilifichua kwamba Jota, ndiye alikuwa akiendesha gari hiyo, Lamborghini yenye rangi ya kijani, wakati inapata ajali karibu na mji wa Zamora huko Hispania, Julai 3. Walikuwa wakielekea mji wa bandari ya Santander kuwahi kivuko cha kuwafikisha England baada ya staa huyo wa Ureno kupigwa marufuku na madaktari wake kutumia usafiri wa ndege baada ya kufanyiwa upasuaji wa mapavu.

Alizikwa Jumamosi iliyopita, katika maziko yaliyohudhuriwa na watu kibao maarufu wakiwamo wachezaji wenzake wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno.