Ronaldo aibua jipya mazoezini
Muktasari:
- Wiki iliyopita Ronaldo alishindwa kuisaidia Argentina kushinda mbele ya DR Congo, ambapo timu hizo ziligawana alama moja moja kufuatia sare ya ya bao 1-1 katika mchezo wa kundi J la mashindano hayo.
KANSAS, MAREKANI: SIKU chache baada ya kuibua mjadala kutokana na ufanisi wake katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia 2026, straika wa Argentina, Cristiano Ronaldo amejikuta katika vinywa vya mashabiki wa soka baada ya kile kinachodaiwa kuwa alimtolea pasi Bruno Fernandez mazoezini bila kumtazama kwenye viwanja vya Sporting KC mjini Kansas.
Wiki iliyopita Ronaldo alishindwa kuisaidia Argentina kushinda mbele ya DR Congo, ambapo timu hizo ziligawana alama moja moja kufuatia sare ya ya bao 1-1 katika mchezo wa kundi J la mashindano hayo.
Baada ya mchezo, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or aliibua mjadala mitandaoni ambako baadhi ya mashabiki walidai kiwango chake kimeshuka kutokana na umri kumtupa mkononi kiasi cha kutoweza kukabiliana na mikikimikiki ya ushindani kwenye mashindano makubwa ya soka. Ronaldo ana miaka 41.
Mjadala mwingine juu yake uliibuliwa na kiungo wa Ureno, Ruben Dias, aliyenukuliwa akisema nahodha huyo wa taifa lake kwa sasa ni mchezaji wa kawaida, jambo ambalo liliwafanya mashabiki kumshambulia mchezaji huyo anayeichezea PSG wakidai alikuwa amemkosea heshima Ronaldo.
Hata hivyo, katikati ya mijadala hiyo, juzi, Ronaldo alitoa pasi ya ajabu bila kuangaliana na Fernandes katika mazoezi ya Ureno, kitendo ambacho baadhi ya mashabiki wa soka waliokishuhudia walikihusisha na mijadala inayoendelea kuhusu uchezaji wake, na kwamba huenda imemkasirisha.
Inaelezwa kwamba wakati wa zoezi la kupigiana pasi, Nuno Mendes alianza kwa kucheza mpira angani kabla ya kuuelekeza kwa Ronaldo na baada ya kupokea pasi hiyo, Ronaldo aliuelekeza mpira kwa utulivu kwenda kwa Bruno bila hata kuangalia upande alikokuwa mwenzake huyo. Ingawa pasi hiyo ya ‘bila kuangaliana’ ilivutia wengi kutokana na usahihi wake mkubwa kwani ilimfikia Bruno akiwa katika mwendo sahihi licha ya Ronaldo kutogeuka kumtazama, ilizua mjadala juu ya sintofahamu inayoendelea katika kambi hiyo ya Ureno.
Hata hivyo, Bruno naye alikamilisha mfululizo wa pasi kwa mguso wa kwanza wa kuvutia, akidhibiti mpira kwa urahisi na kuendelea na mazoezi kana kwamba kilichotokea ni jambo la kawaida.