Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyad Mahrez, El Kaabi wakabana koo AFCON

MAHREZ Pict

Muktasari:

  • Pia Amaodou Haidara wa Mali aliyepewa katika mechi dhidi ya Comoros, hatatumika katika mechi ya 16-Bora dhidi ya Tunisia iliyopangwa kupigwa kesho, wakati Abdoul Moumini wa Benin mwenye kadi mbili za njano atalikosa pambano la Jumatatu dhidi ya Misri.

NYOTA wa Algeria, Riyad Mahrez, sambamba na Brahim Diaz na Ayoub El Kaabi wote wa Morocco wanachuana katika orodha wa wafungaji mabao katika michuano ya 35 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea huko Morocco.

Wachezaji hao watatu wanaongoza orodha ya wafungaji wakiwa na mabao matatu kila mmoja, wakifuatiwa na nyota wengine 13 wenye mabao mawili kila mmoja, huku takwimu zikonyesha kuwa, jumla ya mabao 87 yamefungwa katika mechi 36 zilizochezwa hadi kumalizika kwa hatua ya makundi, huku wachezaji wanne wakijifunga.

Mabao hayo 87 kupitia mechi hizo ni wastani wa kufungwa mabao 2.42 kwa kila mechi, huku timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, ikiongoza kwa kufunga mabao manane, ikifuatiwa na Algeria na Senegal zikiwa na mabao saba, ilihali wenyeji Morocco ikiwa na sita.

Katika mechi hizo 36 za hatua ya makundi, Botswana na Comoros ndizo pekee zilizoaga michuano hilo bila kufunga bao lolote. Botswana pia inaongoza orodha ya timu zilizoruhusu mabao mengi ikifungwa saba kama ilivyo kwa Uganda na Gabon, kisha Zimbabwe na Guinea ya Ikweta zikifuata kwa kufungwa mabao sita kila moja.

MAH 01

Orodha nyingine ya wachezaji 47 wapo nyuma wa vinara wa mabao wakiwa wamefunga bao moja moja wakiwamo Feisal Salum, Charles M’Mombwa na Simon Msuva wa Tanzania, huku nyota wengine wanne akiwamo Saulo Coco wa Guinea ya Ikweta, Aubrey Modiba wa Afrika Kusini, Ghislain Konan wa Ivory Coast na Nene wa Msumbiji ndio pekee waliojifunga katika michuano hiyo hadi sasa.

Saulo alijifunga dhidi ya Sudan, wakati Mobida alijiweka katika mechi dhidi ya Zimbabwe wakati Konan alijifunga mbele ya Cameroon na Nene alijifunga pia dhidi ya Cameroon, huku jumla ya wachezaji saba walilimwa kadi nyekundu katika mechi hizo 32, watatu kati ya hao timu zao zimetinga 16 Bora hivyo kushindwa kutumika.

MAH 02

Wachezaji watakaoshindwa kuzitumikia timu zao katika 16 Bora kutokana na kutumikia adhabu za kadi ikiwamo nyekundu ni pamoja na nahodha wa Senegal, Kalidou Koulibaly aliyepewa dhidi ya Guinea ya Ikweta.

 Koulibaly sasa atalikosa pambano dhidi ya Sudan lililopangwa kupigwa kesho Jumamosi.

Pia Amaodou Haidara wa Mali aliyepewa katika mechi dhidi ya Comoros, hatatumika katika mechi ya 16-Bora dhidi ya Tunisia iliyopangwa kupigwa kesho, wakati Abdoul Moumini wa Benin mwenye kadi mbili za njano atalikosa pambano la Jumatatu dhidi ya Misri.